Na Mapuli Misalaba
Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania
(AICT Dayosisi ya Shinyanga Zakayo Bugota amewakumbusha wakristo kuendelea
kumtumainia Mungu katika maisha ya kila siku
Ameyasema hayo leo wakati akihubiri kwenye ibada ya
Jumapili katika Kanisa la AICT Kambarage mjini Shinyanga ambapo amesema ni
muhimu kila mtu kuwa na matumaini mapya kwa Mungu Mwaka huu 2024.
Amewahimiza wakristo kuwa sehemu ya kugusa maisha ya
watu wengine kwa majitoleo yao huku akiwaomba watanzania kuwa wabunifu katika
maisha ya kila siku wawapo katika Familia, Biashara pamoja na kazi mbalimbali
kama sehemu ya kuimarika kiuchumi.
Askofu Bugota amewaasa wakristo kuendelea kuliombea
Taifa la Tanzania kuepukana na athari zitokanazo na majanga ya mvua huku
akiwakumbusha kujijengea utaratibu wa kumshukuru Mungu hasa wawapo katika
Nyumba za ibada.
Post a Comment