" RC MNDEME AFANYA ZIARA KUKAGUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI SHULENI NA WALE WANAORIPOTI KIDATO CHA KWANZA MANISPAA YA SHINYANGA.

RC MNDEME AFANYA ZIARA KUKAGUA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI SHULENI NA WALE WANAORIPOTI KIDATO CHA KWANZA MANISPAA YA SHINYANGA.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wanaowazuia watoto wao kuripoti shuleni kwa ajili ya kuendelea na elimu ya sekondari hasa wanaotarajiwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka huu 2024.

Ameyasema hayo leo Jumatatu Januari 8,2024 wakati akitembelea baadhi ya shule katika Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kukagua zoezi la uandikishaji wa wanafunzi  wa elimu ya awali,Darasa la kwanza na wale wanaoripoti kidato cha kwanza ambapo ziara hiyo ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.

RC Mndeme amewataka wazazi na walezi kupeleka watoto shule kwani serikali  imeandaa mazingira  wezeshi ya walimu kufundisha na wanafunzi kujifunzia sanjari na elimu kutolewa bila malipo huku akisema hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaowaficha watoto wao.

“Watoto ni haki yao kupata elimu niwaombe wale wazazi ambao bado hawajawapeleka watoto wawapeleke shule nafasi bado zipo muda bado upo lakini kuanzia siku ya leo Tarehe 8 tunaanza masomo rasmi vi vyema sasa mtoto akaanza na wenzake kuanzia siku ya kwanza”

“Hawa watoto wanaoanza na elimu bure tunawaambia wazazi wasahau suala la  ada Dkt. Samia Suluhu Hassan amekwisha lichukua, niwaombe tu wazazi wasiwaweke watoto nyumbani hasa wale wazazi ambao wengine wanawatoto wenye ulemavu wasiwaweke nyumbani kwa sababu miundombinu yote yakuwapokea watoto wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu serikali imeiandaa kwahiyo wazazi wawalete watoto wapate haki yao ya elimu”.amesema RC Mndeme

Aidha mkuu wa Mkoa huyo amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kuepuka mambo yasiyofaa yanayoweza kukwamisha malengo yao katika elimu ambapo amewahimiza kuwaheshimu walimu wao na kuzingatia mambo mazuri wanayofundishwa shuleni hali ambayo itachangia pia kuwaepusha na mmomonyoko wa madili.

Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mwalimu Dafroza Ndalichako amesema maandalizi yote ya kuwapokea wanafunzi wenye sifa za kuanza Mhula mpya wa Masomo kwa Mwaka 2024 yamekamilika.

Kwa upande wao watoto walioanza Masomo leo wameipongeza serikali kwa kuwawekea miundo mbinu rafiki ya kujifunzia huku wakiahidi kusoma kwa bidii.

Kwa upande wao walimu wakuu wa shule za Msingi na wakuu wa sekondari wamesema mwitikio wa watoto wenye sifa za kuanza mhula wa masomo 2024 unaridhsha.

Takribani Watoto 47,187  kati ya 75,079  Mkoani Shinyanga wameandikishwa kuanza darasa la awali kwa Mhula mpya wa  masomo 2024 huku wanafunzi 44332 kati ya 69,792 wakiandikishwa kuanza Darasa la kwanza na wale wote waliochaguliwa kuanza  kidato cha kwanza.Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika shule ya awali na msingi Mwenge Manispaa ya Shinyanga leo Jumatatu Januari 8,2024

Post a Comment

Previous Post Next Post