Na
Mapuli Misalaba, Misalaba Media
Serikali
imewataka watumishi wa afya kutoa huduma bora kwa wananchi wakiwemo Mama
wajawazito, kwa kuzingatia misingi na maadili ya utumishi wa umma.
Hayo
yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambae
pia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bwana Mobhare Matinyi kwenye
Mkutano na Waandishi wa Habari ambao umefanyika leo Ijumaa Januari 5,2024 jijini
Dar Es Salaam.
Amesema utoaji wa huduma bora kwa wa Mama wajawazito
utasaidia kupunguza vifo wakati wa kujifungua na kwamba serikali kupitia wizara
ya afya tayari ina kitengo maalum kinachofuatilia vifo vya Mama mjamzito
Nchini.
Matinyi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa
za kituo ama mtumishi wa afya anayekwenda kinyume na maelekezo ya serikali
ikiwemo kutoza fedha wa Mama wajawazito wakati wa kujifungua ambapo suala hilo
serikali imepiga marufuku.
Post a Comment