" SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA AFYA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.

SERIKALI YAWATAKA WATUMISHI WA AFYA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.

 

Na Mapuli Misalaba, Misalaba Media

Serikali imewataka watumishi wa afya kutoa huduma bora kwa wananchi wakiwemo Mama wajawazito, kwa kuzingatia misingi na maadili ya utumishi wa umma.

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambae pia ni Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bwana Mobhare Matinyi  kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari ambao umefanyika leo Ijumaa Januari 5,2024 jijini Dar Es Salaam.

Amesema utoaji wa huduma bora kwa wa Mama wajawazito utasaidia kupunguza vifo wakati wa kujifungua na kwamba serikali kupitia wizara ya afya tayari ina kitengo maalum kinachofuatilia vifo vya Mama mjamzito Nchini.

Matinyi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa za kituo ama mtumishi wa afya anayekwenda kinyume na maelekezo ya serikali ikiwemo kutoza fedha wa Mama wajawazito wakati wa kujifungua ambapo suala hilo serikali imepiga marufuku.

Post a Comment

Previous Post Next Post