" SHIRIKA LA AKILI PLATFOM TANZANIA LATEMBELE KITUO CHA WAZEE IPULI NA KUPANDA MITI 145

SHIRIKA LA AKILI PLATFOM TANZANIA LATEMBELE KITUO CHA WAZEE IPULI NA KUPANDA MITI 145

Shirika la Akili Platfom Tanzania Jumamos Januari 6, 2024 Uongozi wa Shirika hilo kwa kushirikiana na vijana kutoka vyuoni wamefika katika kituo cha wazee ipuli kwa jina lilizoeleka Kijiji cha Amani kwa zoezi la kutenda matendo ya huruma ikiwa ni pamoja na kupanda miti 145 ya matunda na migomba kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Akili platfom Tanzania Ceo.Mc.Mwl.Roghat Robert ametaja malengo ya shughuli hiyo ikiwemo kuwafariji wazee na kuwatakia maisha marefu katika Mwaka huu 2024

 “Tumeamu kutembelea kituo hiki kama sehemu ya kufungua mwaka 2024 kwa kupata baraka za wazee, Kupanda miti ambayo itatoa faida kwa wazee hasa kuwapatia matunda, kivuli, hewa safi na kuzuia mmonyonyoko wa aridhi, Kutoa mwangaza kuwa matendo ya huruma ni sehemu ya ibada na kazi za mikono kwani kupitia kufanya kazi hufungua mwanya zaidi, Kuwafariji wazee na kuwatakia maisha marefu kwa mwaka huu wa 2024 lakini pia Kuonyesha mchango wa vijana katika kusaidia wenye uhitaji maalum akitolea mfano wa vijana kutoka chuo kikuu cha AMUCTA, TPSC na chuo cha  ARIDHI Tabora ambao ni chachu kuu ya kuonyesha faraja, matumaini, amani na matumaini kwa wenye uhitaji”. amesema Mkurugenzi Roghat Robert

 Kwa upande wake Bi Pendo Chiryamkubi amesema,vijana wanatakiwa kuendelea kutambua dhamana na wajibu wao  katika kusaidia wazee na makundi mengine maalum katika jamii.

 “Hivi leo vijana   kutoka shirika  letu pendwa sana linaloongozwa na vijana wadogo ila mambo makubwa la Akili Platform Tanzania mmeonyesha mfano bora wa kuigwa kwa kuweka alama katika kituo cha wazee na wasiojiweza Ipuli kwa kupanda miti ya matunda itakayosaidia wazee kupata matunda, kivuli na hewa ndani ya kituo chetu ni alama isiofutika na haijawahi tokea tangu kituo kimeanza kituo hiki nitafikisha taarifa wizarani waone mlivyo fungua mwaka 2024 kwa ubunifu mkubwa sana hakika tumuombee kiongozi wetu bw. roghat robert anapambana mkiungana naye vizuri mtafika mbali kila mmoja atambue mchango wake”.amesema B. Pendo

 Katika hatua nyingine Bi. Upendo msimamizi wa kituo cha wazee amesema hakika imekuwa neema kwani  serikali imesha andaa mazingira ya kuwajengea nyumba wazee na zaidi miti ya matunda itasaidia katika eneo la lishe baada ya kustawi vizuri.

 “Zaidi italeta mazingira mazuri kwani hakuna aliyeweza kuleta bustani zaidi ya Wadau wa Akili platfom Tanzania kwakweli Mungu awape maisha marefu taarifa hii na mimi nafikisha wizarani”.

 “Niwaombe sana mtakuwa mnakuja kuijulia hali ili tukiwa pamoja haitakufa hata mmoja endelea kuleta miti bado uhitaji ni mkubwa sana hasa hii ya matunda”. 

 Naye mwenyekiti wa mtaa wa uredi Ndg. John Mwanda ameonyesha kufurahia ustawi wa vijana katika matendo ya huruma na kusema hii ni tunu na hazina daima ameomba kupandiwa miti mingine kwenye shule zake huku akisema atahakikisha miti ilipandwa anaisimamia vyema na inazaa matunda chanya.

 Huku Mzee Edward Sonda amesema baraka ziwashukie vijana na watu wazima waliweza kujitoa katika kufanikisha shughuli ya kuwafikia na kuwawekea bustani kama ya Adam aliyokuwa akisimamia  kwa niaba ya wazee wote.

“ Tunashukuru sana kwa kila mlichotuwezesha hakika nyie ni tunu uzee kuzeeka nasi tulikuwa vijana pia”.

 Bi. Amina ni mdau wa mazingira na anapenda mazoezi ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wazee kwenye kutuo hicho kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha mwili na fya zao.

 Vijana wamesema wataendelea kujitoa zaidi katika kuwasaidia wazee pamoja na watu wengine wenye mahitaji maalum.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post