Na Mapuli Kitina Misalaba
Shirika lisilo la kiserikali la Compass Tanzania limegawa
miche ya miti mia mbili (400) katika kata ya Itwangi pamoja na kata ya Nsalala
Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za
serikali katika hatua za utunzaji wa mazingira.
Akigawa miche hiyo Afisa maendeleo wa kata ya Tinde
Bi. Eva Mlowe amesema serikali inatambua mchango unaofanywa na mashirika
yasiyoyakiserikali kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili jamii.
Afisa maendeleo amepongeza juhudi za shirika la Compass
Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono maono ya serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira.
“Shirika
la Compass Tanzania nimekuja wakati muafaka tunajivunia uwepo wa shirika hili
katika kata ya Tinde kwa sababu ninaenda sambamba na sera ya Nchi kwa kweli
wanamuunga mkono Mama Samia kwa kuifanya Tanzania kuwa ya kijani kwa kutunza
mazingira”.amesema Afisa maendeleo Bi. Eva Mlowa
Mtendaji wa kata ya Nsalala Paul Kulwa amelishukuru
shirika la Compass kwa kutoa miche ya miti mia mbili (200) ambayo waliomba ili
wapande katika mazingira ya kata hiyo huku akiahidi kuilinda ili iweze kustawi
vizuri.
Kata ya Nsalala miti hiyo itapandwa katika shule ya msingi
Nshishinulu, Zahanati mpya ya Nshishinulu pamoja na ofisi ya kata ya Nsalala.
Aidha kata ya Itwangi miche hiyo itapandwa shule ya sekondari
Imenya pamoja na Zahanati ya Butini
iliyopo kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Kwa upande wake meneja miradi wa shirika la Compass Tanzania Bwana Boniface Mhana amesisitiza juu ya utunzaji wa miti hiyo huku akiahidi kutembelea kwenye vituo ambavyo vimepanda miti ili kufuatilia hatua za ukuaji wa miti hiyo.
Meneja huyo amesema shirika la Compass Tanzania kuanzia Mwezi Disemba
Mwaka 2023 hadi Januari Mwaka huu 2024 limegawa
miche ya miti 5000 kama sehemu ya kutunza na kuhifadhi mazingira.


Post a Comment