Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga
Mamlaka ya majisafi na
usafi wa mazingira Shinyanga (SHUWASA) imefanikiwa kukamata wezi wa maji
wapatano 76 kati ya Mwaka wa fedha 2021/2022 na Mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo
wamekadiriwa adhabu inayofikia zaidi ya Milioni 29.
Hayo yamebainishwa leo
Alhamis Januari 4,2024 na Mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA Mhandisi Yusuph
Katopola kwenye mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika katika ukumbi
wa mikutano wa SHUWASA uliopo ofisi kuu za SHUWASA mjini Shinyanga.
Mkurugenzi huyo pamoja na
mambo mengine amesema SHUWASA kwa kipindi hicho imefanikiwa kukamata wezi wa
maji 76 huku akiwataka wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo mengine kuacha
tabia hizo ambapo amesema mamlaka hiyo itaendelea kuwachukulia hatua kali watu
watakaobainika na wezi wa maji.
Tumefanikiwa
kukamata wezi wa maji wapatano 76 kati ya Mwaka wa fedha 2021/2022 na
Mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo wamekadiriwa adhabu inayofikia 29,161,858. Amesema Mkurugenzi Mhandisi Katopola
Mhandisi Yusuph Katopola
amesema mamlaka hiyo pia imefanikiwa kupunguza changamoto ya upotevu wa maji
kutoka asilimia 26 kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 hadi asilimia 20 kwa Mwaka wa
fedha 2022/2023.
Pia SHUWASA Mwaka 2021/2022 ilifanikiwa kupata tuzo ya mamlaka bora katika mamlaka Ishilini na sita (26) za Mikoa katika hatua za udhibiti wa upotevu wa maji kwa kuwa na upotevu wa asilimia 16 ambapo Mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia Mwezi Disemba 2023 mamlaka hiyo ilikuwa na upotevu wa maji asilimia 11.
Post a Comment