UONGOZI wa
Simba umeweka wazi kuwa watawashtua wengi
kwa mashine za maana watakazoshusha kupitia usajili wao wa
dirisha dogo ambao umelenga kuboresha kikosi hicho kwenye mechi za ushindani.
Ipo wazi kwamba
2023 Simba ilifunga kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma KMC
2-2 Simba na mabao yalifungwa na Saido Ntibanzokiza na Jean Baleke ambaye
kafikisha mabao 8 kwenye ligi, yale ya KMC yalifungwa na Wazir Junior.
Meneja wa
Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameliambia Spoti Xtra kuwa
mpaka Januari 15 watakuwa wamshatambulisha wachezaji wapya ambao watakuwa
kwenye kikosi hicho kuongeza nguvu.
“Kwenye usajili wetu
wa dirisha dogo nina uhakika tutawashtua wengi kutokana na aina ya wachezaji
ambao tutawatambulisha, hawa wanakuja kufanya kazi kweli ukizingatia kwamba
dirisha dogo halihitaji kusajili wachezaji wengi.
“Maboresho ambayo
yanafanyika kwenye dirisha dogo ni maalumu kuongeza nguvu maeneo ambayo
hayakuwa imara kidogo kutokana na sababu mbalimbali lakini tutawambulisha
wachezaji wapya kabla ya Januari 15 mashabiki watawatambua,” alisema Ally.
Tayari Simba imetoa zawadi
ya mwaka mpya 2024 kwa mashabiki wake baada ya kumtambulisha nyota mpya, Salehe
Karabaka ambaye anakuwa ni mchezaji wa kwanza
kutambulishwa ndani ya Simba kupitia dirisha hili dogo.
Stori na Lunyamadzo Mlyuka
Post a Comment