
Imeandaliwa na idara ya habari SMAUJATA Wilaya ya Kahama.
Shujaa wa Maendeleo na
Ustawi wa jamii Tanzania (SMAUJATA) mkoani Shinyanga wametakiwa kuendelea
kujikita zaidi katika kufanya kazi kwa vitendo na sio maneno pamoja na kuwa
wazalendo kwa kuibua vitendo vya ukatili wa kijinsi vinavyofanyika kwa
wanawake, watoto na wazee mkoani humo.
Kauli hiyo ametolewa na kaimu mkuu wa wilaya ya Kahama JOSEPH MKUDE
wakati wa viongozi wa SMAUJATA walipokuwa wakitambulisha baadhi ya viongozi
wapya wa wilaya Kahama kwa mwaka 2024, huku wakiombwa kufanyakazi kwa kujitoa
ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii inatuzunguka.
Aidha, MKUDE amesema kuna
kila sababu serikali kuwa na ushirikiano na SMAUJATA kupinga na kufufua vitendo
vya ukatili vinavyoendelea katika mkoa wa shinyanga pamoja kutoa elimu kwa wananchi
ili kupunguza ama kutokomeza ukatili huo ambao una athari kubwa kwa jamii
ambapo waathrika wakubwa ni wanawake, watoto na wazee.
“Sisi ni watu wa
kijitolewa na tufanyekazi kwa vitendo kwa ajili ya nchin yetu, tukubali kufanya
kazi kwa kuwa tatizo ni kubwa sana kuliko tunavyofikiria kwa hiyo tunapaswa
kufanya kazi kweli kweli, alisema Mkude.
Naye, mwenyekiti wa
SMAUJATA mkoa wa Shinyanga NABILI KISENDI, amesema kuwa kumekuwepo na
changamoto ambazo wakati mwingine wanashindwa kufika maeneo ya mbali hasa
vijiji hali inayosababisha kushindwa kuibua vitendo vya ukatili na kuomba
serikali kuendelea kutoa ushirikiano namna ya kufika maeneo hayo.
Amesema kuwa wameendelea
kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika wilaya tatu za mkoa wa
shinyanga kwa kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi, mashuleni pamoja kwenye
vikao vya wakina mama vikoba, pamoja na kuwataka SMAUJATA kupaza sauti kwa
kupinga ukati na kutomeza.
Kwa upande wake kaimu
afisa tawala wa wilaya ya kahama VICENTI NDESEKIO katika kikao hicho alisema
kuwa jukumu la kupinga ukatili wa kijinsi ni la pamoja na kupambana
kulitokomeza na pia kuwataka waendelee kufanya kazi hizo ya kizalendo ili
kuokoa kizazi kijacho katika kutoa elimu ya mmonyonyoko wa maadili.
Menyekiti wa maadili
SMAUJATA mkoa wa Shinyanga SOLOMONI NAJULWA almaafu CHEUPE, ameomba viongozi wa
SMAUJATA mkoani humo wawaze kutambuliwa kwenye sherehe, makongamano na mikutano
ya kiserikali ili waweze kutoa elimu pamoja na kutoa vizuizi kwa baadhi ya
taasisi za kiserikali kama vile hospitali na mashuleni na ili kuweza kutekeleza
majukumu yao ya kupinga na kutokomeza ukatili kijinsia.
“Ofisi za mkurugenzi
pamoja na maafisa ustawi na maendeleo ya jamii mkoa wa shinyanga zinapaswa
kuwatambua SMAUJATA na kupewa heshima zote kana kwamba wao ni sehemu ya chombo
ambacho kinaweza kumasidia Dkt Rais SAMIA HASANI pamoja na wandaamizi wote kwa
kumaanisha sisi ni jukumu letu la kupambana kwa kuporomoka kwa maadili alisema
Najulwa.
Hata hivyo katibu wa
SMAUJATA mkoa wa shinyanga DANIEL KAPAYA alisema mpaka sasa wana kampeni ya
miaka mitatu toka mwaka 2022, yenye lengo la kupinga na kutokomeza ukatili wa
kijinsia nchi nzima ambapo wanashirikiana na maafisa maendeleo ya jamii na
ustawi wa jamii pamoja na viongozi wote wa serikali ikiwa chini ya wazira ya maendeleo
ya jamii jinsia na wanawake na makundi maalum Dr DOROTHY GWAJIMA.
Kikao cha pamoja cha viongozi wa SMAUJATA Mko wa Shinyanga na kaimu mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Joseph Mkude kikiendele.
Picha ya pamoja
|
|



Post a Comment