" TUZINGATIE USAFI KWA AJILI YA AFYA ZETU

TUZINGATIE USAFI KWA AJILI YA AFYA ZETU


Wananchi wa Kijiji cha Mwigumbi, kata ya Mondo iliyopo Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kufanya usafi na kujenga vyoo ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.

Elimu hiyo ilitolewa Januari 25, 2024 na Mkaguzi Kata wa Kata ya Mondo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Huruma Aloyce alipotembelea kaya 40 katika Kata hiyo.

Mkaguzi Huruma alisema kuwa kati ya kaya 40 alizotembelea alikuta kaya 30 hazina vyoo jambo ambalo linahatarisha afya za wakazi wa kata hiyo.

Sambamba na hilo Mkaguzi Huruma alitoa wito kwa wananchi wote wa Kata hiyo kujenga vyoo vya kudumu ili kuepukana na athari za magonjwa ya mlipuko yatokanayo na kutokufanya usafi na kutokuwa na vyoo bora katika maeneo yao.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post