
Uchaguzi huo umefanyika katika Kanisa la International Evangelical Assembilies of God (IEAGT) ambao umesimamiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Mkoa wa Shinyanga Mchungaji David Hamad pamoja na Katibu wa umoja huo Mkoa Mch. Sondole.
Wasimamizi wa
uchaguzi huo wamewatangaza viongozi walioshinda ambapo Mwenyekiti wa
umoja wa makanisa ya Kipendekoste Wilaya ya Shinyanga ni Pr. Thomas
Batenga kutoka kanisa la FPCT na kwamba Makamu Mwenyekiti ni
Winifrida Kashumba wa kanisa la IEAGT huku Katibu wa umoja huo Wilaya ya
Shinyanga ni Mch. Selemani wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG)
Wajumbe wengine
waliochaguliwa ni Mch. Benjamin Mayunga wa kanisa la HOSANA pamoja na Mch. Boni
wa kanisa la New Harvest Ministry.
Katika mahubiri
yake Askofu Valelian Kway wa Deeper Life amewataka viongozi waliochaguliwa
kuendelea kuwa waaminifu katika maneno na matendo yao ikiwa ni pamoja na kuwa
wabunifu ili kufikia malengo ya umoja wa makanisa hayo.
Kwa upande wake
Askofu Mkuu David Mabushi wa kanisa la IEAGT amewaasa viongozi hao
kuzingatia muda na malengo ya umoja wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania(
CPCT) katika kuwatumikia waamini wa makanisa hayo.
Naye Mwenyekiti wa
CPCT Mkoa wa Shinyanga Mch. David Hamad kutoka kanisa la Agape Life,
amewasistiza viongozi waliochaguliwa kufuata Katiba na kuweka taratibu bora za
kuwaunganisha Wachungaji wote wa Kipentekoste na Madhehebu mengine ili umoja
huo uweze kuimarika zaidi.
Aidha amewakumbusha
Viongozi waliochaguliwa kuendeleza uhusiano mwema kati ya CPCT na Serikali ya
wilaya ya Shinyanga, Halmashauri na vyombo vya ulinzi.
Mwenyekiti Pr.
Thomas Batenga amewashukuru wajumbe kwa kumwamini katika nafasi hiyo ambapo
ameahidi kuitumikia vema nafasi hiyo huku akiwaomba ushirikiano ili kufikia
malengo yaliyokusudiwa.
Wajumbe
waliohudhuria uchaguzi huo wamepongeza kwa mwendelezo wa kuchaguza
viongozi bora na kuwatakia viongozi wao baraka za Mungu.
Post a Comment