Na Mapuli Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema
jumla ya wagonjwa 18 kati y wagonjwa 41 wameathirika na vimelea vya kuhara na
kutapika Mkoani Shinyanga.
Ameyasema hayo leo Jumanne Januari 9,2024 wakati
akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya ugonjwa wa kuhara na kutapika ulioibuka
hivi karibuni na kusadikiwa vifo vya watu watano katika kata ya Kagonjwa
Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Amesema wagonjwa 41 kati yao 18 wamebainika
kuathirika na vimelea vya ugonjwa wa kuhara na kutapika katika maeneo mbalimbali
ya Mkoa wa Shinyanga.
RC Mndeme ameeleza kuwa tayari Mkoa umeunda timu maalumu ya kuratibu
na kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huo ambapo mpaka sasa zipo kambi tatu za
kufanya matibabu ya ugonjwa huo ambazo ni kituo cha Afya Ihapa katika Manispaa
ya Shinyanga, kituo cha Afya Kagongwa Manispaa ya Kahama na kituo cha Afya
Kishapu Halmashauri ya Kishapu.
“Mnamo
tarehe 28.12.2023 Mkoa wetu katika kata ya Kagongwa Halmashauri ya Manispaa ya
Kahama vilitokea vifo 5 ambavyo vilisababishwa na kuhara na kutapika, hali hiyo
ilipelekea Mkoa kufanya ufuatiliaji katika eneo la Kagongwa Halmashauri ya
Manispaa ya Shinyanga”.
“Mkoa
umeunda timu ndogo ya wataalam ya kuratibu na kufuatilia mwenendo wa ugongwa
huu ambayo tayari imeanza kazi, aidha kwa kila Halmashauri timu kama hizi
zimeundwa na kusimamiwa kikamilifu ili kuzuia kusambaa na kuenea kwa ugonjwa
huu hatari”.
“Mpaka
sasa tunakambi tatu za kufanya matibabu ya ugonjwa huo ambazi ni kituo cha Afya
Ihapa katika Manispaa ya Shinyanga, kituo cha Afya Kagongwa Manispaa ya Kahama
na kituo cha Afya Kishapu Halmashauri ya Kishapu”.amesema
RC Mndeme
Amesema wagonjwa 30 tayari wameruhusiwa ambapo mpaka
sasa wagonjwa watano (5) bado wanaendelea na matibabu kwenye vituo na kwamba
kituo cha afya katika Manispaa ya Kahama wapo wagonjwa wwili, kituo cha Afya
Kishapu wapo wagonjwa wawili na kituo cha afya Ihapa Manispaa ya Shinyanga yupo
mgonjwa mmoja.
Mhe. Mndeme amefafaua kuwa mpaka sasa hakuna vifo
vinavyotokana na ugonjwa wa Kipindupindu na kwamba vifo vya watu waanne (4)
wametoka kwenye jamii na mtu mmoja amefariki akiwa katika Zahanati binafsi
ambapo wote hawakufanyiwa vipimo.
“Kwa
kifupi ugonjwa wa kuhara na kutapika husababishwa na watu kula Kinyesi kibichi
kupitia vyakula au vinywaji na kuenezwa kwa haraka na hivyo huweza kusambaa kwa
muda mfupi zaidi”.
“Dalili
za ugonjwa huu ni kama vile kuharisha mfululizo na mgonjwa kuishiwa maji
mwilini ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kutumia maji yasiyochemshwa, kula
matunda bila kuosha na maji masafi na tiririka, kula chakula cha baridi au
kiporo, matumizi hafifu ya vyoo, utunzaji mbaya wa vyakula pamoja na usafi duni
wa mazingira”.
“Ugonjwa
huu unawea kuepukika kwa kutumia maji safi na salama, kuepuka kula vyakula
vilivyopoa, kutumia maji yaliyotiwa dawa ya Aqwa tabs pamoja na matumizi sahihi
ya vyoo bora”.amesema RC Mndeme
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
ametaja shughuli zinazoendelea kutolewa katika kuhakikisha Mkoa unakuwa salama
ili kujikinga na ugonjwa huu ikiwemo upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa
ajili ya kutolea huduma kwa wananchi, kuhakikisha wahisiwa wanafuatiliwa pamoja
na ndugu au waliokuwa pamoja na wagonjwa (contacts).
Amesema mikakati mingine inayotumika ni pamoja na
kutoa elimu juu ya namna nzuri ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo
kuhara na kutapika, kutumia wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kutembele kaya na
kutoa elimu ya namna nzuri ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara
na kutapika, kufanya vipimo vya maji katika visima mbalimbali katika
Halmashauri zilizoathirika na ugonjwa a kuhara na kutapika, kuwasafirisha
wagonjwa kutoka maeneo yao ya awali kwenda katika vituo vya matibabu pamoja na
kutoa huduma za tiba kwa waliogundulika kuwa n ugonjwa huu.
Post a Comment