" WANAFUNZI WA CHUO CHA ST JOSEPH’S TAWI LA SHINYANGA WATEMBELEA WAGONJWA, KUFANYA USAFI NA KUCHANGIA DAMU SALAMA KATIKA KITUO CHA AFYA KAMBARAGE

WANAFUNZI WA CHUO CHA ST JOSEPH’S TAWI LA SHINYANGA WATEMBELEA WAGONJWA, KUFANYA USAFI NA KUCHANGIA DAMU SALAMA KATIKA KITUO CHA AFYA KAMBARAGE

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya wanafunzi wa chuo  cha mtakatifu Joseph (St Joseph’s) tawi la Shinyanga  wamefanya zoezi la usafi wa mazingira, uchagiaji damu salama pamoja na kutembelea wagonjwa katika kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha mtakatifu Joseph tawi la Shinyanga Ridhiwani Ramadhani amesema baadhi ya wanafunzi hao wameguswa na kuamua kuunga mkono kampeni ya uchagiaji damu salama ili kusaidia wenye uhitaji.

Ametumia nafasi hiyo kuziomba taasisi mbalimbali na jamii kwa ujumla kuwa na  utaratibu wa kuchagia damu salama kwani itasaidia  kuokoa watu wenye uhitaji wa damu salama.

Rais huyo wa serikali ya wanafunzi katika  chuo cha mtakatifu Joseph tawi la Shinyanga Ridhiwani Ramadhani pia ameikumbusha jamii kuendelea kuzingatia usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu.

Baadhi ya wanafunzi na viongozi wengine wa serikali ya wanafunzi katika chuo hicho ambao wameshiriki zoezi la uchangiaji damu salama pamoja na usafi wa mazingira kwenye kituo cha Afya Kambarage wamesema watandelea kuwa na majitolea kwa watu wenye uhitaji.

Wataalam wa Maabara Devotha Omary pamoja na Mansoor Mbarouk  wamewashukuru na kuwapongeza wanafunzi wa chuo cha mtakalifu Joseph kwa kuchangia damu salama pamoja na kufanya usafi katika mazingira yanayozunguka  kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga.

Mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu Joseph tawi la Shinyanga akichangia kutoa damu salama katika kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga.


Post a Comment

Previous Post Next Post