Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kitaifa ya upimaji wa darasa la nne na kidato cha pili uliofanyika mwaka 2023 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.13 kwa kidato cha pili na asilimia 0.39 kwa darasa la nne.
Akitangaza
matokeo hayo leo Jumapili, Januari 7, 2024 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Said
Mohamed amesema baraza hilo limefuta
matokeo kwa wanafunzi 178 wa darasa la nne na 28 wa kidato cha pili waliofanya
udanganyifu.
Pia
baraza limewafutia matokeo wanafunzi watatu wa darasa la nne na 14 wa kidato
cha pili walioandika matusi.
Aidha
amesema katika masomo ya darasa la nne, matokeo yanaonyesha ufaulu wa sayansi
na teknolojia ukifikia asilimia 86.86 kutoka asilimia 83.19 ya mwaka 2022 na
somo la hisabati likifiki asilimia 54.00 kutoka asilimia 49.7.
Kwa
kidato cha pili, ufaulu wa somo la uraia umeimarika kutoka asilimia 31.12 mwaka
2022 hadi kufiki asilimia 48.27.
Katibu
huyo amefafanua kuwa matokeo ya darasa
la nne, wanafunzi 1,287,934 sawa na asilimia 83.34 wamefaulu kuendelea na
darasa la tano.
Lakini katika upande wa kidato cha pili, wanafunzi 592,741 ambao ni sawa na asilimia 85.31 wamefaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne.
Post a Comment