" WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUKARABATI DARAJA KATA YA NDEMBEZI SHINYANGA, MENEJA WA TARURA MHANDISI GILBERT AELEZA HATUA ZILIZOPO

WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUKARABATI DARAJA KATA YA NDEMBEZI SHINYANGA, MENEJA WA TARURA MHANDISI GILBERT AELEZA HATUA ZILIZOPO

TAZAMA VIDEO HII.

Na Mapuli Misalaba, Moshi Ndugulile

Wakazi wa kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wamewaomba wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA Mkoa wa Shinyanga kukarabati daraja linalounganisha mawasiliano ya kata hiyo na maeneo mengine ambalo limekatika kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.

Wakizungumza na Misalaba Media ilipotembelea katika daraja hilo wamesema kuharibika kwa daraja hilo imekuwa ikikwamisha shughuli za kiuchumi kutokana na kukatika kwa mawasiliano kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Wamesema changamoto hiyo inahusisha pia wanafunzi wanaotumia daraja hilo ambao wamekuwa wakichelewa masomo darasani  kwa sababu ya kuzunguka.

Wananchi hao wameiomba TARURA kutengeneza daraja hilo kwa kiwango chenye ubora ili liweze kudumu kwa muda mrefu kwani limekuwa likitengenezwa na kuharibika mara kwa mara hivyo kuitia hasara serikali.

Misalaba Media imezungumza na meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA Mkoa wa Shinyanga mhandisi Oscar Gilbert kwenye eneo la tukio ambaye ameahidi kushughulikia changamoto hiyo ili kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaotumia daraja hilo.

Hata hivyo injinia Gilbert amesema mpango uliopo ni kuwasiliana na mamlaka ya reli kwa kuwa daraja hilo limejengwa kwenye hifadhi ya reli.

Daraja hilo linalounganisha Ndembezi Mazinge na Ndembezi Bushimangila limekatika hivi karibuni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Mwananchi akivuka katika daraja  linalounganisha Ndembezi Mazinge na Ndembezi Bushimangila kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.





Meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA Mkoa wa Shinyanga mhandisi Oscar Gilbert akiangalia hali ya changamoto katika daraja  linalounganisha Ndembezi Mazinge na Ndembezi Bushimangila kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.





Post a Comment

Previous Post Next Post