Wajariamali wanawake
mkoani Morogoro wamewaomba wadau wa ukuzaji wa biashara kutoishia mijini na
kufika kwenye vijijini kutoa elimu na usaidizi wa ukuzaji biashara ili
kuwajengea uwezo kuzalisha bidhaa zenye ubora unaokubalika na zinazoweza
kukabili ushindani wa soko ya ndani na nje ya nchi.
Wajasiriamali hao
waliyasema hayo jana wakati wakiongea kwenye mafunzo ya wajasiriamali wanawake
kuhusu kanuni, taratibu na sheria za kufanyabiashara kwenye soko la Afrika
(AICFTA) yaliyoandaliwa na Chemba ya wafanyabiashara wanawake Tanzania (TWCC)
ulifanyika mjini hapa.
Mmoja wa wajasiriamali
hao Eva Kipalile mkazi wa Kijiji cha Mbingu kata ya Igima Wilayani Mlimba
alisema, licha ya kuzalisha vikapu, ungo na mazao aina ya Kakao lakini
wanakabiliwa na changamoto ya kukosa masoko ya nje kutokana na kukosa nembo ya
kuhakiki ubora (TBS), Misimbomilia(Barcods) na usajili wa urasimishaji biashara
kutoka BRELA.
“watu hao wanapaswa
kufika vijijini kwetu na wasibaki mjini, sababu leo tumejifunza vitu vingi,
wenzetu wanaweza kutoka kwenda kufanya biashara na mataifa mbalimbali lakini
sisi tunashindwa kutoka sababu hatuna vitu ambavyo ni muhimu na tumevijulia
hapa” alisema Kipalile.
Naye Makamu Mwenyekiti wa TWCC Taifa Rose Romanus alisema ajenda yao ni kuhakikisha wanawake wanamiliki pesa kwa kutimiza malengo waliyojiwekea kwa kulifikia soko huru la Afrika.
Akifungua mafunzo hayo
Katibu tawala Msaidizi upande wa biashara, viwanda na uwekezaji mkoani hapa
Beatrice Njawa aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuchangamkia
fursa zinazotolewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuzalisha bidhaa zenye ubora
zinazokidhi viwango vya masoko likiwemo soko huria la Afrika linalohudumia nchi
54.
Post a Comment