Watu tisa wamefariki katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kiromo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani baada ya Coaster ya Abiria ikitokea Dar es salaam kuelekea Bagamoyo kugongana uso kwa uso na Lori lililobeba mawe likitokea Bagamoyo kuelekea Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar kunenge ametoa pole kwa majeruhi na Ndugu waliofiwa na kuwakumbusha Madereva kuwa makini kwa kufuata sheria wanapokuwa barabarani.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Halima Okash amewapa pole Wananchi wa Bagamoyo na kuwashukuru Wananchi wa Kiromo kwa kutoa msaada kwa Majeruhi “waliofariki ni Wanaume saba, Wanawake wawili, Majeruhi ni Wanaume wawili na Mwanamke mmoja”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Pius Lutumo amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa lori kutaka kulipita gari jingine kwenye eneo lisiloruhusiwa.
CHANZO - IDAWA MEDIA
Post a Comment