Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ameendelea kuwaonya watu wanaotumia shida za wengine kama fursa ya kujinufaisha.
Askofu Sangu ametoa onyo hilo kupitia mahubiri aliyoyatoa leo kwenye Misa ya Dominika ya matawi, iliyofanyika kijimbo katika Kanisa kuu la Mama mwenye huruma Ngokolo mjini Shinyanga, ikiwa ni hatua ya kutaka kuona jamii nzima inaishi kwa upendo, haki na kuwajali wengine.
Askofu Sangu amebainisha kuwa, bado kuna baadhi ya watu wakiwemo wakristo wanaendelea kufanya dhuluma kwa kutumia shida za watu wengine kama fursa ya kujinufaisha, hasa pale ambapo wau wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo wagonjwa, yatima na wajane wanapohitaji huduma au msaada wowote kupitia kwenye mikono yao.
Amewataka wale wanaomwamini Kristo wayaone mateso aliyoyapata katika safari ya kumkomboa mwanadamu kupitia nafsi za wengine hasa wanaopitia changamoto mbalimbali ikiwemo, wagonjwa, wafungwa magerezani, yatima na wajane na kwamba, wanapaswa kuwaonyesha upendo kama Kristo mwenyewe alivyokuwa na upendo kwa wanadamu na kukubali kuteswa na kufa Msalabani kwa ajili yao.
Askofu Sangu ameitaja hatua ya kutumia shida za wengine kuwa ni dhambi kubwa na ni chukizo mbele za Mwenyezi Mungu.
Katika hatua nyingine, Askofu Sangu amewakumbusha Wakristo wote kuendelea kujiweka karibu zaidi na Mungu kwa kusali na kutubu dhambi zao kupitia Sakramenti ya kitubio pamoja na kuacha kukimbilia mafundisho ya uongo ambayo yamejengwa katika misingi ya miujiza badala ya kuwapeleka watu kwa Mungu.
Leo, Kanisa Katoliki kote ulimwenguni linaadhimisha Dominika ya Matawi, ambayo ni kumbukumbu ya kupokelewa kwa Yesu Kristo kwa shangwe mjini Yelusalemu, siku chache kabla ya kukamatwa, kusulubiwa na kufa msalabani na baadaye kufufuka siku ya tatu.
Askofu Sangu akibariki Matawi kupitia Ibada ya kubariki Matawi iliyofanyika nje ya Kanisa
Askofu Sangu akibariki matawi ya waamini
Shemasi James Chingila anayefanya utume wake katika Kanisa kuu Ngokolo akisoma somo a Injili
Askofu Sangu akitoa Homilia baada ya kubariki matawi
Maandamano ya kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendelea na adhimisho la Misa takatifu
Misa inaendelea
Bi.Suzana Masanja akisoma somo la kwanza
Wanakwaya wakiimba kwenye Misa
Bw. Jofrey Madirisha akisoma somo la pili
Shemasi James Chingila pamoja na baadhi ya waamini walioandaliwa kwa ajili ya kusoma Historia ya mateso ya Yesu
Askofu Sangu akitoa Mahubiri mara baada ya kusomwa kwa Historia ya Mateso ya Yesu
Waamini wakimtolea Mungu sadaka zao
Wanajumuiya ya zamu wakileta matoleo
Askofu Sangu akipokea matoleo
Misa inaendelea
Waamini wakiwa Kanisani
Misa inaendelea
Walelewa wa Shirika la Kijimbo la Maria Mtakatifu Mama wa Huruma wakiwa Kanisani
Watawa wakiwa Kanisani
Misa inaendelea
Askofu Sangu akiwakomunisha waamini
Paroko wa Parokia ya Ngokolo Padre Adolf Makandagu akiwakomunisha waamini
Askofu Sangu akimkominisha katibu wa Halmashauri walei Jimbo Mwl.James Msimbang’ombe
Waamini wakiendelea kukomunika kupitia Watawa
Mwl.James Msimbang’ombe ambaye pia ni Katibu wa Halamshauri walei Jimbo na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri walei Parokia ya Ngokolo akitoa Matangazo kwa ajili ya adhimisho ya Juma kuu
Misa imekwisha maandamano kutoka Kanisani huku Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akitoa baraka kwa waamini