BARAZA LA MADIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA LAMTAKA MKURUGENZI KUWA NA TAKWIMU YA WAWEKEZAJI


Na Mapuli Kitina Misalaba

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga limemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa na takwimu sahihi ya wawekezaji ili kunufaika na miradi ya wajibu kwa jamii CSR  hasa katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Maelekezo hayo yametolewa  Machi 6,2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2023\2024.

Mhe. Mboje ameyasema hayo baada ya Madiwani wa Halmashauri hiyo kuhoji kwa Mkurugenzi hali ya ukusanyaji wa mapato kwa wawekezaji katika migodi hasa Mwakitolyo pamoja na Mwenge ambao kwenye taarifa ya Mkurugenzi hawakubainishwa kuwa sehemu ya wajibu kwa jamii CSR.

“Wajumbe hawakuweza kuridhishwa na orodha kwahiyo tunachokihitaji ni orodha ya wale wawekezaji  na namna gani Halmashauri inanufaika orodha ya wawekezaji ambao Baraza liliwahitaji hawapo lakini pia ule unufaika kwa sasa ni kidogo tunataka wawekezaji ambao Baraza liliwahitaji wawekwe ili tulinganishe idadi ya wawekezaji waliopo na kile tunachokipata vinawiana”.

“Mtendaji wa kata alikuja nikampa orodha ya makampuni yote yaliyowekeza kwenye kata yangu ya Mwakitolyo sasa leo hii siyaoni kwenye maadhimio kwanza ni zaidi ya makampuni manne mimi najisifu kwamba kata yangu ni kata ya wawekezaji lakini ninapokuja kwenye Baraza siyaoni sasa haya makampuni yanapita pitaje”.

Mpaka sasa Halmashauri hiyo imefikia asilimia takribani 40 ya ukusanyaji wa mapato kwa Mwaka wa Fedha 2023\2024 ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje ametumia nafasi hiyo  kumuelekeza Mkurugenzi na wataalam wake kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ikiwa ni pamoja na kuongeza vyambo vya mapato ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

“Wewe unajua kabisa kuwa mapato hamko vizuri lakini Madiwani wanaoishi kule kwenye hizo kata wamekuonyesha wawekezaji lakini haujatoa ushirikiano tunataka kujua mpaka sasa umechukua hatua gani kama umewaagiza wataalam wako kwenda kuchukua orodha na wameshaichukua Diwani ametoa ushahidi kuna shida gani mpaka sasa orodha ya makampuni bado haijakufikia wakati watendaji walichukua orodha mi nadhani kuna udhaufu mkubwa kwenye ukusanyaji wa mapato inawezekana siyo wewe Mkurugenzi ila wale wataalam wako wanaokusaidia kwahiyo unatakiwa uchukue mawazo yetu kwamba sisi tumeona kunashida unatakiwa kuchukua hatua kwa wahusika, mimi naagiza tu kwamba atuletee hatua alizochukua kwa wahusika ambao wamechukua orodha Mwakitolyo mpaka sasa hawajaiwasilisha kwake”.amesema Mwenyekiti Mboje

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesisitiza kuwa ni vema Halmashauri hiyo kuweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na Madiwani kuhakikisha  zoezi la ukusanyaji mapato linafikia malengo ambapo ameagiza siku ya Ijumaa wiki hii kupata orodha ya wawekezaji wote katika Halmashauri hiyo ili hatua zaidi zianze kuchukuliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini Mhe. Edward Ngelela naye amehimiza kila kata kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika zoezi la ukusanyaji wa mapato.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba ameahidi kushughulikia maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa kwa lengo la kuleta matokeo chanya ambapo amesema kuwa tayari amewaelekeza watendaji kutoka kwenye kata, kuhakikisha wanahudhuria kwenye vikao vya Baraza la Madiwani ili kuepusha changamoto inayojitokeza hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Aidha Madiwani kutoka  Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Shinyanga wamewasilisha taarifa mbalimbali za kata zao huku  wakitaja changamoto mbalimbali ikiwemo  ya ubovu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo kwenye kata zao pamoja na uhitaji wa Zahanati kwenye vijiji.

Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuanza mchakato wa kutoa Fedha kwa ajili ya kumalizia jingo la kituo cha Polisi kata ya Iselamagazi ambayo ni ahadi ya Halmashauri hiyo kutoa Milioni kumi kwa ajili ya kumalizia boma lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Ametoa agizo hilo baada ya diwani wa kata ya Iselemagazi kuhoji ukamilishwaji wa boma lililoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

“Sisi tunajengo hapa la kituo cha Polisi ambalo lilijengwa kwa nguvu za wananchi Halmashauri iliahidi kutoa Milioni kumi na dhani ni Miaka sita au Mitano iliyopita na tunajua umuhimu wa kituo cha Polisi hapa ni makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga hatuna ulinzi sahihi tunajengo kubwa mno tulishakamilisha kwa maana ya boma lakini sasa niombe ile ahadi ya Milioni kumi tupate ili jingo hilo likamilike”.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo leo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2023\2024.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ngassa Mboje akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo leo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2023\2024.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye Baraza hilo leo Jumatano Machi 6,2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini  Mhe. Edward Ngelela akizungumza kwenye Baraza hilo leo Jumatano Machi 6,2024.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Kisena Mabuba akiahidi kuendelea kutatua changamoto zilizopo.

Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani uliolenga kupokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli  za maendeleo kutoka kwenye kata mbalimbali katika kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2023\2024 ukiendelea leo Jumatano Machi 6,2024.

Diwani kata ya Ilola Mhe. Amosy Mshandete akizungumza kwenye Baraza hilo.

Diwani wa kata ya Salawe Mhe.Joseph Buyugu akizungumza kwenye Baraza hilo.

Diwani wa kata ya Mwakitolyo Mhe. Masalu Nyese akizungumza kwenye Baraza hilo.


Diwani wa kata ya Iselamagazi Mhe. Isack Sengelema akizungumza kwenye Baraza hilo.



 

Previous Post Next Post