CCM WILAYA YA SENGEREMA YAUNGA JUHUDI ZA MBUNGE TABASAM KATIKA UJENZI WA CHAMA.

 

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Agostin Makoye amewaomba wanachama wa chama hicho kumpa ushirikiano Mbunge wa  Jimbo hilo Tabasam Hamis kutokana na utekelezaji wake wa Ilani ya chama hicho kwa asilimia mia moja.

 Makoye ameitoa rai hiyo wakati wa kufungua mafunzo maalumu yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uongozi viongozi kutoka katika kata zote sambamba na kujipanga katika uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na uchaguzi Mkuu ujao mafunzo hayo ambayo yamewashirikisha  viongozi wa chama kutoka kata zote za Jimbo la Sengerema,jumuiya zote pamoja na madiwani wa kata zote za Jimbo hilo.

 

"Kwa kweli alichokifanya Mbunge wetu Mheshimiwa Tabasam ni jambo kubwa sana na la kihistoria hivyo sie kama chama tutampatia sapoti kubwa Mbunge wetu kwakweli amefanya mambo makubwa ata sie kama chama atujawahi kufanya semina kwa viongozi wetu leo hii semina ni ya tatu anafanya ni gharama kubwa kufanyika,Agostin Makoye - Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sengerema.

 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Sengerema  Jackson Mazinzi amesema jumuiya hiyo imeamua kumpa sapoti Mbunge wa Jimbo hilo Tabasam Hamis kutokana na utekelezaji wake katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo,Maji,Barabara,Umeme pamoja na miundombinu mbalimbali.


 

 

 Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis amesema,katika Jimbo hilo ameweza kutekeleza miradi mbalimbali ambayo ilikuwa changamoto kubwa ususani suala la shule za sekondari ambapo kulikuwa na changamoto kubwa katika Wilaya hiyo hivyo kufanikiwa kujenga jumla ya shule za sekondari 17 kwa kushirikisha wananchi.

 "Nataka leo niwambie viongozi wangu zile shule 17 za sekondari nilizoamasisha ujenzi wake nikatoa gari la kubeba mchanga wa ujenzi wa shule hizo, kwasasa serikali imetoa zaidi ya bilioni 1 nukta 7 kukamilisha ujenzi wake kinachofuata sasa ni ujenzi wa shule mbili za msingi kwa kila kata ili kumaliza changamoto ya watoto wa shule hizo kubanana katika chumba kimoja cha Darasa.

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis Mwagao amesema dhamira yake kubwa ni kuhakikisha Wilaya ya Sengerema inaondokana na changamoto zote zilizokuwepo

Previous Post Next Post