DARAJA LA KIGONGO - BUSISI UJENZI WAKE WAFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 90.

 

Na Swalehe Magesa Misalaba Media, Sengerema - Mwanza

" Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan aliachiwa mradi mkubwa wa ujenzi wa Daraja la Busisi Bilioni 730 na mtangulizi wake Hayati John Magufuli,mradi huu unakimbilia asilimia zaidi ya asilimia 90 tumebakiza sehemu dogo sana watu waanze kupita kutoka Kigongo - Busisi wala atukutegemea katika maisha yetu iko siku litapitika kuja hapa watu wapite wakitembea,"Tabasam Hamis - Mbunge Jimbo la Sengerema.


Hayo yamebainishwa na Mbunge huyo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Busisi katika Mkutano wa hadhara ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kusikiliza kero na kuzifanyia ufumbuzi wake kutoka kwa wananchi katika Jimbo la Sengerema na hadi sasa ameweza kuzifikia kata tano za wilaya ya Sengerema.

 


 

Previous Post Next Post