HIZI HAPA 'COMBINATION' MPYA KIDATO CHA TANO

 Hizi Hapa 'Combination' Mpya Kidato cha Tano


Serikali kupitia Ofisi Ya Rais Tamisemi imekamilisha zoezi la awali la kuingiza kwenye kanzidata taarifa zilizo kwenye Fomu za Uchaguzi za wanafunzi kama zilivyojazwa na wanafunzi wakiwa shuleni.

Aidha, napenda mtambue kuwa Mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala ya Elimu kwa Kidato cha Tano yameanza kutekelezwa, ambapo utekelezaji huo umehusisha uanzishaji wa Tahasusi mpya 49, kutoka 16 zilizokuwepo awali hadi kufikia tahasusi 65’

Tahasusi hizo mpya zitakazoanza kutekelezwa Julai, 2024 zipo katika makundi saba (7) ambayo ni: Tahasusi za Sayansi ya Jamii; Tahasusi za Lugha; Tahasusi za Masomo ya Biashara; Tahasusi za Sayansi; Tahasusi za Michezo; Tahasusi za Sanaa; na Tahasusi za Elimu ya Dini.

Zoezi la kubadilisha tahasusi na vyuo limeanza rasmi tarehe 20 Machi, 2024 hadi tarehe 30 Aprili, 2024. Wanafunzi, wazazi na walezi wanakumbushwa kushauriana kikamilifu ikiwa ni pamoja na kupata ushauri wa kitaalam na kitaaluma kabla ya kufanya mabadiliko ya tahasusi au Kozi.

Ninawasisitiza wanafunzi, wazazi/ walezi kutumia muda huo vyema ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa.

Ni muhimu kuzingatia muda uliotolewa wa kufanya marekebisho ili ratiba ya kuwachagua na kuwapangia shule na vyuo iweze kuendelea kwa muda uliopangwa.

Baada ya matokeo ya kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo kutangazwa, Ofisi haitashughulikia changamoto hizo kwa kuwa fursa ya kufanya mabadiliko hayo imeshatolewa amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa.






Previous Post Next Post