Na Mapuli Kitina Misalaba
Afisa bima na mahusiano TCB Bank tawi la Shinyanga
Bi. Neema Frank Mongi amewaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa
wingi kufungua akaunti katika Bank hiyo ili kunufaika na fursa mbalimbali
zitokanazo na TCB Bank.
Amesema kufungua akaunti ya TCB Bank ni bure ambapo
gharama za uendeshaji wa akaunti zipo chini na kwamba hali hiyo itamsaidia
mteja kutunza pesa zake bila wasiwasi.
Afisa huyo wa
bima na mahusiano TCB Bank tawi la Shinyanga Bi. Neema Frank Mongi ametaja
baadhi ya fursa za akaunti katika Bank hiyo huku akiwaomba wananchi wote
kujitokeza kufungua akaunti ili
kunufaika na fursa zilizopo.
“TCB
Bank ina huduma ya akaunt ya wanawake, Inaitwa TABASAMU akaunt, ambayo haina
makato ya Mwenzi ili kumwezesha mwanamke kujitunzia pesa zake Pia kuna akaunt
ya dream akaunt ambayo kwa ajili ya watoto miaka 0 mpaka 18”.
“Ipo
akaunt ya muda maalum inayoitwa WADU Kwa ajili ya kujitunzia pesa kwa malengo
maalum,kwa kiasi ambacho utajitunzia kila Mwezi kwa kadri unavyo weza, TCB Benk
inayoongoza kwa kufungua akaunt kwa masharti nafuu sana na akaunt inafunguliwa
bure kabisa na gharama za uendeshaji wa akaunt zipo chini sana”.
“Zote
hazina makato ya Mwezi,makato ni ukiwa unafanya muamala lakini pia kuna huduma ya bima bima za aina zote, nyumba,magari,
biashara, kilimo pamoja na na bima ya vikundi NISHIKE MKONO ambayo
utapata mkono wa pole wa hadi Milioni tano kwa Elfu 24,000 tu”Amesema Neema
Kwa maelezo zaidi fika TCB Bank tawi la Shinyanga huduma ni nafuu sana.
Afisa bima na mahusiano TCB Bank tawi la Shinyanga
Bi. Neema Frank Mongi akiwaomba wananchi kujitokeza kwenda kufungua akaunti TCB
Bank ili kunufaika na fursa zilizopo.
Afisa bima na mahusiano TCB Bank tawi la Shinyanga
Bi. Neema Frank Mongi akiwaomba wananchi kujitokeza kwenda kufungua akaunti TCB
Bank ili kunufaika na fursa zilizopo.