Kwa mafanikio ya biashara yoyote, eneo ambalo biashara hiyo inafanyika lina machango mkubwa sana. Kuna biashara ambayo inaweza kufanikiwa kwenye eneo moja na ikashindwa kwenye eneo jingine.
Kabla hujaanza biashara yako, ni vyema ukajiridhisha kama eneo unalokwenda kufanya biashara hiyo ni sahihi kwa biashara unayokwenda kufanya. Na ili kujua kama eneo linafaa kuna mambo muhimu unatakiwa kuyafanyia kazi, huamki tu na kusema hapa nitaweka biashara yangu.
Leo kupitia mtandao huu wa napenda biashara tutajadili mambo muhimu sana kwako kuzingatia kuhusu eneo la biashara yako.
Jambo muhimu kabisa la kuzingatia ni kuhusu soko la biashara yako, kuhusu wateja.
Wafanyabiashara wengi hufikiri kujua kama biashara yao ina soko au la ni rahisi sana. Lakini sio kweli. Kujua kama unaweza kufanya biashara eneo fulani kwa kupima soko unahitaji kujiuliza maswali haya muhimu;
Swali la kwanza; Je kuna wateja wa biashara hii?
Hili ni swali muhimu sana unalotakiwa kujua, utakuwa umeamua kushindwa kwenye biashara kama utaamua kuingia bila ya kujiuliza swali hili ambalo litakupa mwanga wa biashara unayokwenda kufanya. Jua kama kuna wateja wa biashara unayokwenda kufanya.
Swali la pili; Je wateja wapo wa kutosha.
Kuwepo tu kwa wateja hakutoshi kukushawishi wewe ufungue biashara kwenye eneo fulani, unahitaji kuwa na wateja wa kutosha kukuwezesha wewe kuendesha biashara yako. kama wateja ni wachache ni vigumu sana wewe kuweza kuendesha biashara kwa faida. Hakikisha wateja waliopo wanaweza kuiwezesha biashara kujiendesha na wewe ukapata faida.
Swali la tatu; Je wateja ni rahisi kufikika au kuifikia biashara yako?
Unaweza kuwa na wateja, na wateja wakawa ni wengi ila wakawa wamesambaa sana kiasi cha wewe kushindwa kuwafikia au wao kushindwa kuifikia biashara yako. ni lazima wateja wako wawe kwenye eneo ambalo ni rahisi wewe kuwafikia au wao kuifikia kwenye biashara yako.
Kama utajiuliza maswali hayo matatu na kujijibu vizuri kulingana na biashara yako, basi utapata mwanga mkubwa sana kuhusu wateja wa biashara yako.
Kitu kingine muhimu sana kuzingatia kuhusu eneo la biashara ni ushindani.
Ushindani ni kitu kitakachokupa mwanga sana kuhusu eneo unalokwenda kuanzisha biashara yako. Na katika kuangalia ushindani unaangalia pande zote mbili;
Upande wa kwanza; kama hakuna kabisa ushindani jua kwa nini.
Usikimbilie kufungua biashara mahali kwa sababu hakuna kabisa ushindani. Jua ni kitu gani kimewafanya wengine wasifungue biashara kama hiyo. Ni nadra sana wewe kuwa ndio wa kwanza kuiona hiyo fursa. Huenda kuna ambao walianza wakashindwa, huenda ni uzembe tu wa watu. Unapojua sababu hasa ni nini, unaweza kujipanga vizuri ili kufanikiwa.
Upande wa pili; kama kuna ushindani mkali jua unaingiaje.
Kama eneo unalotaka kuanzisha biashara lina ushindani mkali sana, kwanza jua kuna soko la kutosha. Kisha jua unaingiaje kwenye eneo hilo. Usiingie kwa sababu umeona kuna wateja, ingia kwa sababu umeona kuna fursa ya wewe kuleta utofauti na ubora ambao wengine hawatoi sasa.
Kitu cha mwisho tutakachojadili hapa ni ukaribu wako na eneo la biashara.
Hakikisha unakuwa karibu na eneo lako la biashara. Usianzishe biashara eneo ambalo ni mbali sana na wewe, itakuwia vigumu kwako kuisimamia vizuri na hivyo kushindwa kufanikiwa.
Hakikisha unatafakari vyema kuhusu eneo la biashara yako, lina mchango mkubwa sana kwenye mafanikio ya biashara hiyo.

Post a Comment