Na
Elisha Petro
Kamati
ya jinsia na walimu wanawake Manispaa ya Shinyanga kwa niaba ya katibu wa chama cha walimu Mkoa
wa Shinyanga (CWT) Mwalimu Alen Shuli imekabidhi
msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha Agape kilichopo Manispaa ya Shinyanga
ili kuwasaidia wanafunzi kuepukana na changamoto mbalimbali zinazowakabiri.
Hayo
yamebainishwa na waalimu akiwemo Mwenyekiti wa kamati hiyo Mwalimu Rose Mabana
wakati wakizungumza na wanafunzi hao katika kituo hicho ambapo amesema msaada
huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Mwenyekiti
huyo amewatia moyo wanafunzi wanaolelewa katika kituo cha Agape na kwamba
amewasihi kuendelea kusoma na kufanya kazi kwa bidii kwa kumtanguliza Mungu na kukitumia kituo hicho kuwa daraja la
mafanikio katika maisha yao.
Akisoma taarifa fupi ya vitu vilivyokabidhiwa Mhasibu wa kamati hiyo Mwalimu
Stella Lucas Halimoja amebainisha baadhi ya vitu vilivyotolewa ikiwemo Mahindi debe tatu, Mchele kilo 60, Maharage kilo
40, Sababu za unga na mche, Unga wa Mahindi, Matunda, Nguo, Viatu na fedha elfu hamsini na mbili (5,2000/=).
Kwa
upande wake mkurugenzi wa kituo cha Agape Bwana John Myola amewashukuru walimu
kwa moyo wa upendo na majitoleo waliyoyafanya ili kuwasaidia watoto hao kupata
mahitaji ya msingi kwani wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa
chakula, upungufu wa walimu na ukosefu wa huduma ya maji ambapo awali walikuwa
wakitumia maji ya SHUWASA lakini kwa sasa yamekatwa kutokana na kushindwa
kumudu gharama ya malipo.
Sanjali
ya hayo baadhi ya wanafunzi wa Agape wameishukuru kamati hiyo kwa kuwa mfano wa
kuigwa katika jamii kupitia msaada walioutoa na kuwaomba waendelee kuwa na moyo
wa kuwasaidia pale wanapohitaji msaada wao.
Kamati
ya jinsia na walimu wanawake Manispaa ya Shinyanga kwa niaba ya katibu wa chama cha walimu Mkoa
wa Shinyanga (CWT) leo Alhamis Machi 7,2024 imekabidhi msaada wa vitu
mbalimbali katika kituo cha Agape kilichopo Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake
Duniani ambayo kilele chake ni kesho Machi 8,2024.