Na Swalehe Magesa, Misalaba Media - Misungwi Mwanza
kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za ustawi na maendeleo ya jamii imetembelea mradi wa ujenzi wa Hostel katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo Kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wake.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi wilayani Misungwi mkoani Mwanza Charles Achuodho amesema ujenzi wa mradi wa Hostel katika chuo hicho ulianza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza kuanzia Mwezi Juni Mwaka jana na ukakamilika mwaka jana Mwezi Novemba katika hatua ya msingi kwa kiasi cha gharama ya shilingi milioni mia tatu ( 300 )
Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ally Hamis amesema mradi wa ujenzi wa Hostel zitasaidia vyuo wa maendeo ya jamii kuchukua wanafunzi katika maeneo mbalimbal ya mikoani hasa wanafunzi wa kike kutokana na kuitajika wataalam wa kike kuwa wahandisi .
Kwa upande wao wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Mbunge wa viti maalum Kabula Enock Shitobela pamoja na wajumbe wengine wa kamati hiyo wameupongeza mradi huo na kusema utasaidia hasa usalama wa wanafunzi watasoma katika chuo hicho kwenda kuishi nje ya maeneo hayo ambayo ni hatarishi.
Post a Comment