" KAMATI YA WANAWAKE TUGHE MKOA WA SHINYANGA YATOA ZAWADI KUPUNGUZA MAHITAJI KITUO CHA AFYA BULUNGWA HALMASHAURI YA USHETU

KAMATI YA WANAWAKE TUGHE MKOA WA SHINYANGA YATOA ZAWADI KUPUNGUZA MAHITAJI KITUO CHA AFYA BULUNGWA HALMASHAURI YA USHETU

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya Wanawake wa Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya TUGHE Mkoa wa Shinyanga leo imetoa  zawadi ya mahitaji mbalimbali ikiwemo Kompyuta pamoja na mzani wa kupimia watoto wachanga katika kituo cha Afya Bulungwa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, ikiwa ni sehemu ya  maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Hafla ya kukabidhi vitu hivyo imefanyika katika  viwanja vya kituo cha Afya Bulungwa ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali na kwamba mgani rasmi ni Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni akimwakilisha Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Chelehani.

Akizungumza kaimu Mwenyekiti wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally Choyelo amesema kamati  hiyo imekuwa na utaratibu kila Mwaka wa kufanya matendo ya huruma kwa kutua huduma katika maeneo mbalimbali na kwamba Mwaka huu wameguswa kupunguza changamoto ya vitendea kazi katika kituo cha Afya Bulungwa.

“Katika kutekeleza hilo tumeona ni vyema sasa tuje tushirikiane na nyie kama Bulungwa kama Ushetu ili tuweze kutoa vile tulivyoviandaa kutoka kwa akina Mama wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga jambo hili siyo mara ya kwanza kulifanya Miaka yote tumekuwa tukijipanga na kutembelea sambamba na kutoa hizi huduma Mwaka jana tumefanya katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na tulienda kutembelea vituo mbalimbali kwahiyo dhima kubwa ni katika kutekeleza sera ya TUGHE kama sulogani yetu inavyosema HUDUMA BORA MASLAHI ZAIDI”.amesema Bi. Mariam

Katibu wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga Catherine Masalu amevitaja vitu hivyo vilivyotolewa na kamati hiyo ya TUGHE Mkoa wa Shinyanga ikiwemo kitambaa cha kijani kwa ajili ya wazazi na huduma za upasuaji ambapo amesema kamati hiyo itaendelea kutembelea Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kufanya matendo ya huruma kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali.

Kama inavyofahamika kwamba kila ifikapo Machi 8 huwa ni maadhimisho ya siku ya Wanawake na sisi kupitia chama cha wafanyakazi TUGHE huwa tunafanya matendo ya huruma kwa jamii na safari hii matendo ya huruma tumeyafanyia katika kituo cha Afya Bulungwa iliyopo Halmashauri ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga”

“Katika kituo hiki tumetoa mahitaji mbalimbali ikiwemo Machine ya kupimia  sukari, Kompyuta mbili (2), Kitambaa cha kijani kwa ajili ya wazazi na huduma za upasuaji, Mzani  wa kupimia watoto  wachanga pamoja na  Roll  moja ya green material”.amesema Bi. Catherine

Mganga mkuu wa Wilaya ya Ushetu Dkt. Athuman Matindo pamoja na mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bulungwa wemeishukuru kamati hiyo ya  chama cha TUGHE Mkoa wa Shinyanga, kwa kuguswa na changamoto za kituo hicho ambapo ameahidi kuvilinda na kuvitumia kama ilivyokusudiwa katika kurahishisha huduma kwa wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni Baluhya naye amewapongeza Wanawake hao kwa majitoleo yao ambapo amesema kuwa ofisi ya Mbunge itatoa mahitaji mengine katika kituo hicho ndani ya Miezi mitatu.

“Mhe. Mbunge amenituma kusema Infusion Mashine ataileta ndani ya Miezi mitatu pamoja na Hormone Analyzer  hizi zitakuja ndani ya Miezi mitatu kwa hatua hii wana Bulungwa tutakuwa tumevuka malengo ya maombi yetu, naomba zawadi hizi ni zawadi zilizogharamikiwa kwa gharama kubwa sana naomba usimamizi wako Mganga mfawidhi wa kituo hiki vifanye kazi lengwa tu, kwa malengo ya wagonjwa tu na wataalam wako naomba kabisa vipokeeni lakini pia vitunzeni”.amesema Mhe. Baluhya

Kwa upande katibu wa TUGHE Mkoa wa Bwana Ramadhan Pangara amemshukuru mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Bulungwa kwa ushirikiano wake katika kubainisha changamoto zilizopo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wafanyakazi ambao bado hawajajiunga na chama hicho waweze kujiunga ili kunufaika na fursa mbalimbali.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Velena Peter wakati akifunga hafla hiyo ameipongeza kamati ya Wanawake wa TUGHE Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa zawadi hizo huku akiwahakikishia kuendelea kufuatilia ahadi za ofisi ya Mbunge kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa changamoto katika kituo cha Afya Bulungwa.

Kamati ya Wanawake wa Chama cha wafanyakazi wa serikali na Afya TUGHE Mkoa wa Shinyanga Machi 11,2024 imetoa  zawadi ya mahitaji mbalimbali pamoja na kutembelea wodi ya wazazi katika kituo cha Afya Bulungwa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, ikiwa ni sehemu ya  maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga Bi. Mariam Ally Choyelo akieleza dhima ya kamati hiyo.

Katibu wa kamati za Wanawake TUGHE Mkoa wa Shinyanga Catherine Masalu akitaja mahitaji yaliyotolewa na kamati hiyo.

Katibu wa TUGHE Mkoa wa Bwana Ramadhan Pangara akiwaomba watumishi wa Afya kujiunga na chama hicho.

Mwenyekiti wa TUGHE Wilaya ya Ushetu Dkt. John Duttu akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni Baluhya akizungumza kwa  niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu.

Mgeni rasmi, Diwani wa kata ya Bulungwa Mhe. Kalwani Mteganoni Baluhya akizungumza kwa  niaba ya Mbunge wa Jimbo la Ushetu.








 

Post a Comment

Previous Post Next Post