KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Ndg.Khadija Ali Salum (pichani kushoto), amefanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini China Khamis Mussa Omar (kulia) kwa lengo la kuendelea kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine wawili hao wamekubaliana kuendelea kuwasiliana kwa mustakabli mzuri wa jamii ya Wazanzibar na Tanzania kwa ujumla.