NA Swalehe Magesa, Misalaba Media - Ilemela, Mwanza
- Bodaboda kushiriki kongamano hilo ili kutoa maoni yao.
- Viongozi wa Vyama vya siasa kushiriki bila kujali hitikadi zao za vyama.
Kongamano
kubwa la Kanda ya ziwa la kutathmini miaka mitatu ya utawala wa Rais
Dkt.Samia Suluhu Hassan maarufu, ( MAFIGA MATATU ) linatarajiwa
kufanyika mkoani Mwanza Machi 30 mwaka huu katika ukumbi wa Kwa Tunza
Beach Resort Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ukumbi wa hotel ya Kwa Tunza Beach Resort
Aloyce Nyanda Mtozi mratibu wa MAFIGA MATATU YA RAIS DKT SAMIA amesema,
TATHMINI
ya miaka mitatu ya utawala wa Rais Dkt,itawakunisha,watu zaidi ya elfu
mbili kutoka Kanda ya ziwa wakiwemo,viongozi mbalimbali, wananchi,vijana
wa vyuoni pamoja na wanachama wa Vyama vya siasa ili waweze kujadili na
kutoa maoni yao kwa uhuru zaidi.
Aidha
ameongeza kuwa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini hiyo ambayo
itatanguliwa na mambo kadhaa ambayo yatafanyika ndani ya wiki moja na
kuyabainisha,
Ambapo
amesema,kutakuwa na matukio kadhaa katika kuelekea tathmini hiyo ya
utawala wa Rais Dkt Samia sambamba na utoaji wa taulo za kike kwa watoto
wa kike mashuleni,wanafunzi wa Vyuo vikuu na Vyuo vya kati kutoka Kanda
ya ziwa watatembelea Miradi ya kimkakati,
Vile
siku ya Jumatano Machi 27 litafanyika zoezi la upandaji wa miti ambalo
litahusisha vyama vyote vya siasa vilivyopo hapa nchini katika zoezi
hilo.