HomeKIMATAIFA MANCHESTER CITY KUWAKARIBISHA NEWCASTLE UNITED HATUA YA ROBO FINALI MICHUANO YA FA CUP. Misalaba March 15, 2024 0 Na Elisha PetroMarch 16,2023 jiji la Manchester viunga vya Etihad Pep Gurdiola atawaongoza vijana wake kulikabili jeshi la Eddie Howe (Newcastle United) katika mchezo wa robo fainali kombe la FA.Manchester City hawajapoteza michezo yao 19 waliyocheza hivi karibuni wakiwa nyumbani uwanja wa Etihad na hawajafungwa toka 6/12/2023 walipofungwa na Aston Villa na tayari michezo yao 21 iliyopita bila kupoteza.Edie Howe na Newcastle yake anakazi kubwa kuwazuia Manchester City wamekuwa na matokeo ya kuchanganya wanaweza kupoteza unapowaamini na wanaweza kushinda usipotarajia lakini kwenye michezo migumu wamekuwa wepesi sana rejea mchezo wa Chelsea, Arsenal na Manchester City wenyewe hawaonyeshi ugumu kama msimu uliopita.Newcastle kwenye michezo yao mitano ya mwisho katika mashindano yote wameshinda mchezo mmoja dhidi ya Wolves sare michezo miwili (Bournemouth na Blackburn kwenye FA wao wakisonga mbele kwa mikwaju ya penalty 4-3),michezo minne yote wameruhusu bao. Michezo mitano ya mwisho kati ya Manchester City dhidi ya Newcastle Pep amekuwa na matokeo mazuri kwani kashinda michezo mitatu yote ya ligi kuu kapoteza mchezo mmoja wa Carabao Cup na kapata sare mchezo mmoja nao wa ligi kuu.Kabla ya mchezo wa Manchester City dhidi ya Newcastle United utakaochezwa saa 2:30 usiku kutatanguliwa na mchezo kati ya Wolves dhidi ya Coventry majira ya saa 9:15 alasiri. You Might Like View all
Post a Comment