MBUNGE VITI MAALUM MKOA WA SHINYANGA DKT. CHRISTINA MZAVA ATEMBELEA SHULE ZA SEKONDARI NA KUZUNGUMZA NA WANAWAKE WAJASILIAMALI

Na Moshi Ndugulile

Mbunge  wa viti maalumu Mkoa wa Sinyanga Dkt Cristina Mnzava amefanya ziara ya kikazi ambapo  ametembelea Shule za Sekondari pamoja na kukutana na makundi ya wanawake wajasiliamali katika kata za Lubaga na Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga

Akizungumza na wanafunzi  katika Shule za sekondari Lubaga na Mwawaza zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dkt Mnzava amewataka Wanafunzi hao wasichana na wavulana  kuweka juhudi zaidi katika masomo ili kujiweka katika nafasi nzuri kitaaluma na  kuongeza kiwango cha ufaulu

Amewasisitiza wanafunzi hao kuendelea kuwa waadilifu kwa Wazazi,walimu na jamii inayowaunguka ambapo amewatahadharisha kutojihusisha na mapenzi katika umri mdogo, matumizi ya pombe,Dawa za kulevya na kuepuka tabia na mazingira yote yenye viashiria hatarishi vinavyokwenda kinyume na maadili ya kitanzania ikiwemo usagaji, mapenzi na ndoa za jinsia moja,kwani itawaharibia mwelekeo wa maisha na kuwasababishia fedheha.

 Dkt Mnzava ametoa zawadi ya Madaftari na kalamu kwa Wanafunzi wote waliopata ufaulu wa Daraja la kwanza na la pili

Aidha ameahidi kutoa jezi na vifaa vya michezo kwa timu za mpira wa miguu na mikono kwa timu za wasichana na wavulana katika Shule ya sekondari ya Lubaga.

Amewaomba Walimu kuendelea kushirikiana na Wazazi na walezi kufuatilia na kusimamia mienendo ya Watoto kwa kuwa ni muda mrefu zaidi wamekuwa wakishinda nao.

“Walimu ongeeni na watoto kuhusu afya ya uzazi hali itakayowasaidia kuepukana na mhemko wa rika balehe, tunaamini shuleni ni mahali salama kwa usalama wao” amesema Mnzava  

Kwa upande wake Mwenyekiti wa U.W.T  Mkoa wa Shinyanga Bi Grace Bizuru  ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi hao kuongeza juhudi katika masomo ili kujiweka tayari kuingia kwenye soko huria la wasomi ambapo wanahitajika wataalamu wa taaluma mbalimbali.

Katikataarifa yake kwa Mbunge Dkt Mnzava,Mkuu wa Shule ya Sekondari Lubaga Mwalimu Hamisa Boniface licha ya kueleza mafanikio mbalimbali amesema shule hiyo ambayo ni ya kutwa ina kidato cha kwanza na cha pili na kwamba ilianza mnamo Mwaka jana 2023.

Amesema shule hiyo ina jumla wanafunzi 254 wakiwemo wavulana 127 na wasichana 127,  Walimu 11 kati yao wa kiume ni 8 na wakike 3 hakuna upungufu wa Walimu, na kwamba shule hiyo ilijengwa kupitia fedha za mradi wa uboreshaji Elimu Nchini (sequip)

Mwalimu Hamisa amesema hali ya taaluma shuleni hapo ni nzuri hali ambayo Mkuu huyo wa shule amesema inachangiwa na walimu kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri,kutoa adhabu kwa wanafunzi wanaofanya vibaya mitihani,kudhibiti utoro unasababisha ufaulu hafifu.

Ametaja changamoto kadhaa zinazohitaji kupata ufumbuzi kwamba ni kutokuwa na vifaa vinavyotosheleza kwenye michezo ikiwemo jezi, hali inayopunguza hamasa ya wanafunzi kushiriki michezo, na kutokamilika kwa baadhi ya miundombinu ya shule.

 Akizungumza kwenye ziara hiyo mjumbe wa Baraza la UWT Bi. Christina Gule amesema kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye Mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 wanawake wanapaswa kushiriki kikamilifu  kwa kuchangamkia fursa za uongozi.

Katika ziara hiyo Mbunge Dkt Chrstina Mnzava ametoa madaftari (counter book) matano na kalamu kwa kila mmoja wa wanafunzi waliopata ufaulu wa daraja la kwanza na pili katika mitihani yao ya Mhula ili kuwahamasisha wengine kuongeza juhudi katika masomo,ametoa taulo za kike box kumi kwa wanafunzi wa kike,lakini jezi na vifaa vya michezo kwa shule ya Sekondari Lubaga.

 

Mbunge huyo pia ametoa majiko ya gesi kumi na tano kwa Mama lishe wa kata ya Lubaga na kumi na tano mengine kwa Mama lishe wa kata ya Mwawaza lengo ni kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na kwamba ni njia ya kudhibiti ukataji miti holela kwa ajili ya matumizi ya kuni.

Aidha akiwa katika kata ya Mwawaza amemwongezea Mtaji wa Biashara ya mboga mboga Mama Helena Mabula na wakati huo huo amemwezesha Mkulima wa mbogamboga Bi Julietha kafumu fedha kwa ajili ya kununua mbegu ili kuimarisha shughuli yake hiyo.

Amewataka Wanawake kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fursa mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo fedha kwa ajili ya kufanya shughuli za ujasiliamali

Katika ziatra yake hiyo Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Dkt Christina Mnzava alifuatana na baadhi ya viongozi wa U.W.T ngazi ya Mkoa na Wilaya.


Previous Post Next Post