Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Sengerema Mwanza
Mgombea
udiwani Kata ya Buzilasoga Wilaya ya Sengerema kupitia Chama cha
Mapinduzi Chama cha Mapinduzi Edina Godwin Bandihai ameshinda nafasi
hiyo kwa kupata kura 5227
Edina
amewashinda wagombea 8 wa vyama vya upinzani vilivyoshiriki kwenye
uchaguzi huo mdogo uliofanyika kufuatia kifo cha diwani aliyekuwepo
marehemu Devid Shilinde.
Akitangaza
matokeo hayo saa 5.35 usiku ya uchaguzi huo mdogo katika Kata hiyo ya
Buzilasoga msimamizi wa uchaguzi huo,Binuru Shekidere amemtangaza
mgombea Edina Godwin Bandihai wa Chama cha Mapinduzi kuwa mshindi kwa
kupata kura 5227
Mgombea wa Chama cha ADC Mahuja Mathias Lubinza ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 242 kwenye uchaguzi huo.
Wagombea
wengine pia walioshiriki kwenye uchaguzi huo mdogo ni pamoja
na,Ramadhani Omary Saidi wa chama cha UDPD amepata kura 1,Deus Kavilondo
Nkwabi chama cha NLD kura 6,Msafiri Josephat Mwinyitanga kura 6,Saidi
Ramadhani Abdul kura 7,Anna Sulwa Nzengo chama cha CCK amepata kura 12
na Rehema Hussein Herry chama cha AAFP amepata kura 40
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo mshindi wa uchaguzi huo
Edina Godwin Bandihai wa CCM amewashukuru wananchi wa Kata ya Buzilasoga
kwa kumuamini na kumchagua hivyo ameahidi kuwalipa maendeleo wananchi
wa Kata hiyo.