Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho ataongoza Misa ya Dominika ya Matawi katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa Katibu wa Akofu Padre Paul Mahona, Misa hiyo itaanza saa 2:00 asubuhi na itatanguliwa na Ibada ya kubariki matawi itakayofanyika nje ya Kanisa.
Dominika ya matawi huadhimishwa na Kanisa Katoliki kote ulimwenguni kama sehemu ya kumbukumbu ya kupokelewa kwa Yesu Kristo kwa shangwe mjini Yelusalemu, siku chache kabla ya kukamatwa, kusulubiwa na kufa msalabani na baadaye kufufuka siku ya tatu.
Dominika ya Matawi huadhimishwa wiki moja kabla ya Jumapili ya Pasaka.