MRADI WA BBT WAWANUFAISHA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA WILAYANI BARIADI MKOANI SIMIYU KWA KUONGEZA TIJA KATIKA KILIMO HICHO.


 

Wakulima wa zao la Pamba Bariadi mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuwaletea vijana wa Mradi wa Jenga  kesho iliyo Bora ( BBT ) kwa kuwapatia elimu ya kilimo bora ya zao la pamba ambayo imewasaidia kupata mavuno mengi.


 Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Bariadi Simiyu.

Wakulima hao wakizungumza na Jambo Digital katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye  mashamba ya pamba yaliyopo katika kijiji cha Penyasosi wilayani humo wamesema, awali walikuwa wakipanda mbegu za pamba shambani ya bila kufuata mistari hali ilyopelekea kupata mavuno machache.

 

" Tangia wamekuja hawa vijana wa BBT na kuanza kutoa elimu ya kilimo bora cha zao la pamba tumekuwa na mabadiliko makubwa katika mashamba yetu mavuno yameongezeka sana tumelima hekali chache lakini mavuno ni mengi,"George Buluba - Mkulima wa kijiji cha Penyasosi.

"Kabla ya kupewa elimu hii ya kilimo cha pamba nilikuwa na uzoefu ambao nilikuwa nao kulingana na jinsi nilivyoelekezwa na wataalam mbalimbali waliopo katika kijiji hiki,kwakweli elimu waliyonipa hawa vijana wa BBT wamenifundisha jinsi ya upandaji wa pamba kwa kufuata mistari kwa ujumla nimefundishwa utaalam mkubwa sana tofauti na awali,"Piter Mkomba - Mkulima wa kijiji cha Penyasosi.

Afisa kilimo Mradi wa  BBT katika kijiji cha Nguliati Kata ya Nguliati wilayani Bariadi mkoani Simiyu Agineta Ngamba amesema,mradi huo umekuwa na manufaa makubwa katika kijiji hicho kwa wakulima kwa kuwapatia elimu mbalimbali ya kilimo cha zao la pamba na wakulima wamekuwa na mwitikio mkubwa.


Previous Post Next Post