Na Mapuli Kitina Misalaba
Mtu mmoja Mwanaume anayekadiriwa kuwa na
umri wa Miaka 30 hadi 35 ambaye bado hajafahamika majina yake wala makazi amefariki
Dunia kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya naironi kwenye mti katika kitongoji Wiligwamabu
kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Misalaba Media imezungumza na Mwenyekiti
wa kitongoji hicho Bwana Juma Kulwa Mahona amesema tukio hilo limetokea Machi
4,2024 majira ya saa moja na nusu.
Mwenyekiti huyo amesema marehemu
alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya naironi ambayo aliifunga kwenye tawi
la mti uliopo pembezoni mwa Barabara.
“Taarifa
hii ya mtu kujinyonga nimeipata majira ya saa moja na nusu nilipigiwa simu na
mwananchi tu wa eneo langu baada ya kupata taarifa hiyo nilifika kwenye tukio
nikakuta baadhi ya wananchi wameshafika kwenye hilo eneo la tukio lakini
wananchi waliokusanyika pale hawakuweza kumtambua mtu huyo mimi nilichukua
hatua za kutoa taarifa kituo cha Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi “.amesema
Mwenyekiti Juma
Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa
Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Janeth Magomi
amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo ambapo amesema mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Aidha Kamanda Magomi ameiambia Misalaba
Media kuwa marehemu ameacha ujumbe wa maadishi akieleza sababu iliyopelekea
kujinyonga kuwa ni ugumu wa maisha baada ya marehemu huyo kuomba msaada wa
kifedha kwa Baba yake mzazi bila mafanikio na kujibiwa kwa lugha ambayo siyo
nzuri.
“Ni
kweli siku ya Jumatatu Tarehe 4 Mwezi wa 3 majira ya saa moja na nusu asubuhi
tulipata taarifa kutoka kwa wananchi ambaye aligundua mtu mmoja kujinyonga
jinsia ya kiumbe ambaye mpaka sasa hivi hatujaweza kupata majina yake ambaye
anakadiriwa kuwa na umri kati ya Miaka 30 hadi 35 na mtu huyo aliacha ujumbe
kwa sababu pembeni kulikuwa na Begi”.
“Aliacha ujumbe ndani ya Begi kwenye Daftari
dogo kwamba ameamua kujinyonga kwa sababu ya ugumu wa maisha alimuomba msaada
wa kifedha Baba yake lakini alimjibu vibaya na kwamba yeye kwao ni Simiyu hakutaja jina lake ila aliandika namba za
simu akasema hizo niza mke wake japo kuwa mpaka sasa hivi Mwanamke huyo bado
hajapatikana mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Manispaa ya
Shinyanga na jeshi la Polisi tunaendelea na uchunguzi”.amesema
SACP Magomi