Na Mapuli Kitina Misalaba
Nyumba zaidi ya kumi zimeezuliwa mapaa kufuatia Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo na mawe kunyesha katika mtaa na kata ya Kitangili
Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa wa
Kitangili Bi. Habiba Jumanne amesema Nyumba hizo zilizoezuliwa wakazi wa maeneo
hayo wamenusurika ambapo hali hiyo imesababisha kukosa sehemu ya kulala pamoja na
chakula.
Ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali pamoja na
wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia wahanga hao ili wapate chakula pamoja na
sehemu ya kulala.
Mvua
kubwa iliyoambatana na upepo ambayo ilinyesha kuanzia saa nne usiku na
kuendelea imefanya madhara makubwa kwenye mtaa wangu imeezua Nyumba 11 na hawa
wakazi wamekosa sehemu ya kuishi wanaomba kwa majirani zao lakini pia na
chakula magodolo yote yamenyeshewa na Mvua inamaana hata upande wa chakula
hawana msaada kwa muda huu”.
“Kwahiyo
wapo wabibi wakongwe kabisa ambao hawapa pa kushika na hawana wa kuwasaidia naiomba serikali au
wadau mbalimbali wenye uwezo waweze kuwaidia hawa wa bibi kuwajengea Nyumba
lakini pia kuwapatia chakula kwa kipindi hiki kigumu”.amesema
Mwenyekiti Habiba