MBUNGE TABASAM AFADHILI MAFUNZO YA VIONGOZI WACCM NGAZI YA MATAWI WILAYA YA SENGEREMA ZAIDI YA MIA TANO.

 


MBUNGE TABASAM AFADHILI MAFUNZO YA VIONGOZI WACCM NGAZI YA MATAWI  WILAYA YA SENGEREMA ZAIDI YA MIA TANO.  

-  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sengerema atoa onyo kwa wanaopitapita kufanya kampeni za Ubunge.

- Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sengeremea amuombea Mbunge Tabasam ulinzi ndani ya chama.

 

 Zaidi ya wanachama mia tano wa Chama cha Mapinduzi kutoka ngazi ya matawi wamepewa semina maalumu yenye lengo la kuwajengea uwezo wa wajibu,majukumu piya kuwapa mikakati ya kushinda uchaguzi Mkuu ujao,mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na chama hicho kwa ufadhili mkubwa wa Mbunge wa Jimbo la Sengerema mheshimiwa Tabasam Hamis Mwagao.

 

 

 

 

 Akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya katika hiyo Mheshimiwa Mark Agostini Makoye akawaasa wanachama hao kuwa mafunzo waliyopewa yaende kuwa chachu ya kuleta mabadiliko na ufanisi katika chama hicho na piya wanapopata nafasi za uongozi waende kutimiza majukumu yao sawasawa.



" Bado nina amini akili yangu bado ina kumbukumbu sawasawa ina uwezo wa kutunza kumbukumbu sijapata maradhi ya akili ya kupoteza kumbukumbu kama aitoshi mtaniambia mliwahi kuliona jambo la namna hii linatokea,"tuseme tu ukweli tangu tuzaliwe tuliona jambo la namna hii linatokea,nataka niwambie Jimbo la Sengerema tuna Mbungekama kuna watu wanapitapita waache, " Mark Agostini Makoye - Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sengerema.


 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sengerema Mark Agostini Makoye amewataka wanachama wa chama hicho wanaotamani kuomba nafasi ya ngazi ya ubunge katika Jimbo la Sengerema waweze kutulia hivyo wasubilie muda wa uchaguzi ukifika mwaka 2025.

 



 Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis Mwagao amewataka viongozi kutoka ngazi ya matawi katika Jimbo hilo waweze kuwa waadilfu,wazalendo kutokana na mafunzo  hayo huku akiwaasa kuepuka migongano ya  madaraka ambayo inaweza kukivuluga chama cha mapinduzi katika maeneo hayo.

 


 Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo ya ngazi ya matawi wamempongeza Mbunge wao Tabasam Hamis Mwagao kwa kuweza kugharamia mafunzo hayo ambayo yamewajengea uelewa mpana katika majukumu yao kwenye maeneo wanayotoka.

Previous Post Next Post