Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Tabasam Hamis amewataka viongozi wa shule Jimboni humo kutafuta mbinu mbadala za kutatua changamoto ya michango inayotolewa na wazazi kwa ajili ya kuwalipia watoto kutokumudu kugharamia kutokana kuwa na vipato vidogo .
Rai hiyo ameitoa wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM ) katika kata ya Nyamatongo wakati akizungumza na wanachama wa kata hiyo baada ya kupokea taarifa ya shule zilizopo katika eneo hilo,Mbunge Tabasam yupo kazini akiendelea na ziara ya kata kwa kata sambamba na kusikiliza kero kutoka kwa wananchi.
'' Hali ni mbaya watu wamelima maji yamejaa wakienda ziwani kuvua mvua inanyesha dagaa zinashindwa kuanikwa, kuna shida za kila namna sasa mkija na michango mingi mingi shule hizi zitabakia maboma matupu bila uwepo wa wanafunzi kwenye shule watakimbia,'' Tabasam Hamis - Mbunge wa Jimbo la Sengerema.
Aidha Tabasam amesema, mkakati wake uliopo kwasasa ni ujenzi
wa shule mbili za msingi katika kila kata lengo
likiwa ni kukabiliana na changamoto kubwa
iliyopo ya watoto kuwa wengi katika chumba kimoja cha Darasa,ambapo jumla
ya shule za msingi 54 mpya zitajengwa katika Wilaya hiyo.