RAIS SAMIA ATOA BILIONI 100 KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI KATA YA KAHUMULO.

 

                                 Na Swalehe Magesa, Misalaba Media, Sengerema - Mwanza

Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza Tabasam Hamis amewambia wakazi wa kata ya Kahumulo wilayani humo kuwa Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Vicktoria ili kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo ambayo imekuwa kero kwa wananchi.

 

Tabasam ametoa kauli hiyo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kahumulo wenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi hao.

Aidha amesema mradi huo utahudumia baadhi ya maeneo mbalimbali ya vijiji vya kata hiyo  ikiwemo kijiji cha Nyetundu pamoja na mwaloni huku akisema kilichobakia kwassa ili mradi huo uweze kuanza kutoa huduma ya maji ni mashine ya kusukuma maji hayo.

 

Mheshimiwa Tabasam amefafanua zaidi kwa kusema mradi huo ulitarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka jana ambapo ameshangazwa na ucheleweshaji wa mashine ya kusukuma huduma hiyo ambayo mamlaka inadai kuwa imeagizwa kutoka Uturuki kitendo ambacho amedai kimekuwa kikichelewesha kwa mradi huo kuanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa kata hiyo.


Previous Post Next Post