SERIKALI MKOANI SHINYANGA KUENDELEA KUYAENZI YALE YOTE ALIYOYAFANYA HAYATI ALI HASSAN MWINYI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameungana na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, viongozi wa Dini na Serikali katika Dua na Sala ya kumwombea Rais mstaafu awamu ya pili hayati Ali Hassan Mwinyi.

Akizungumza baada ya kufanyika kwa Dua na Sala hiyo RC Mndeme amemuelezea hayati Ali Hassan Mwingi alikuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa, Mwalimu na mlezi ambaye ameacha alama.

Amesema Serikali pamoja na watanzania wote wataendelea kumkumbuka na kuyaenzi yale yote aliyoyafanya enzi za uhai wake.

Dua hiyo imeongozwa na Shekhe mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya ambaye amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya maisha ya hayati Ali Hassan Mwinyi hapa Duniani ambapo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo.

Misalaba Media imezungumza na baadhi ya viongozi na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kufanya kwa dua hiyo ambao wametoa pole kwa familia ya hayati Ali Hassan Mwinyi ambapo wamesema wataendelea kutaenzi yale mema aliyoyafanya katika kipindi cha uongozi wake..

Leo ni siku ya nne ya maombolezi kufuatia kifo cha Rais Mstaafu hayati Ali Hassan Mwinyi ambaye amefariki Dunia  Februari 29,2024 na mazishi yake kufanyika Machi 2 nyumbani kwake katika kijiji cha Manga Pwani Unguja visiwani Zanzibar.

Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia akiwa katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salam mahali alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na saratani ya mapafu.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amezaliwa mnamo  Mei 08 Mwaka 1925 katika kijiji cha kivure Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,na amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu Mwaka 1985 hadi Mwaka 1995.

Kiongozi wa dini ya Kikristo akiongoza Sala ya kumuombea Rais Mstaafu wa awamu ya pili Tanzania hayati Ali Hassan Mwinyi.



 

Previous Post Next Post