SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA WAKUTANA, KUZUNGUMZA NA MRATIBU WA WFT – Trst MKOA WA SHINYANGA BI. GLORY MBIA

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga  wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Mratibu kutoka mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT – Trust) Mkoa wa Shinyanga Bi. Glory Mbia (aliyekaa upande wa kushoto) leo Jumanne Machi 26,2024.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Baadhi ya viongozi wa kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga leo wamekutana na kuzungumza na mratibu kutoka mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT – Trust) Mkoa wa Shinyanga Bi. Glory Mbia.

Viongozi hao wa SMAUJATA ni pamoja na Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya, Katibu idara ya Itifaki, uanachama na uenezi SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, Mwenyekiti idara ya Jinsia SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Inspekta Alkwin Willa pamoja na Mwenyekiti wa SMAUJATA Wilaya ya Kishapu Bwana Emmanuel Makolo.

Mazungumza hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga wameendelea na ziara za kutembelea ofisi za serikali, viongozi wa Dini na taasisi mbalimbali ikiweno za binafsi kwa lengo la kutengeneza mahusianio mazuri katika utekelezaji wa majukumu yao ya kupambana na vitendo vya ukatili.

SMAUJATA ni kampeni ya kupinga ukatili Nchini yenye kauli mbiu yake isemayo “KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA” ambapo kampeni hiyo inatekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga  wakiwa katika mazungumzo ya pamoja na Mratibu kutoka mfuko wa Ruzuku wa Wanawake Tanzania (WFT – Trust) Mkoa wa Shinyanga Bi. Glory Mbia (aliyekaa upande wa kushoto) leo Jumanne Machi 26,2024.

 

Previous Post Next Post