Na Mapuli Kitina Misalaba
Viongozi wa Kampeni ya kupinga ukatili ya Shujaa wa
Maendendeleo na Ustawi wa jamii Tanzania ( SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga
wamekutana na mtoto akifanya Biashara ya Miwa ndani ya Basi siku ya shule Manispaa
ya Kahama.
Mtoto huyo wa kike anakadiliwa kuwa na umri wa Miaka
kumi, ameeleza kuwa anasoma shule ya msingi darasa la tano katika Manispaa ya
Kahama.
Baadhi ya wakazi na wafanya Biashara ndogondogo wa
eneo hilo la Manzeze Manispaa ya Kahama wameeleza kuwa mtoto huyo amekuwa
akifanya Biashara hiyo kwa kushirikiana na Baba yake mzazi.
Kwa upande wake Baba mzazi wa mtoto huyo amekili
kuwa amekuwa akimtumia mtoto huyo kuuza Miwa.
Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya
pamoja na katibu idara ya Itifaki, uanachama na uenezi Mkoa wa Shinyanga Bwana
Solomon Najulwa wametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi kuacha mara
moja kuwatumikisha watoto katika umri
mdogo kwani ni kinyume na sheria na taratibu za Nchi.
Aidha wameongeza kuwa mazingira hayo siyo salama kwa
mtoto kwani yanaweza kusababisha athari mbalimbali ikiweko kufanyiwa ukatili.
Pia wamewasisitiza wazazi na walezi kuwaruhusu
watoto kuhudhuria shuleni siku za shule ili wawese kutimiza ndoto zao.
Kwa kuzingatia mapendekezo ya taarifa ya tume Mwaka 2009 Serikali ilitunga sheria ya mtoto sura ya 13 ambayo imeainisha masuala mbalimbali yanayohusu mtoto ambapo sheria inaruhusu mtoto mwenye umri kuanzia Miaka 14 kufanya kazi nyepesi zisizohatarisha Afya, Elimu na maendeleo yake na kwamba sheria inazuia kumshawishi, kumlazimisha au kumshurutisha mtoto.