Na Elisha Petro
Michuano ya Jamukaya Ramadhani Cup msimu wa 2024 inatarajia kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa SHYCOM uliopo Mkoani Shinyanga kwa timu 16 kuwania ubingwa wa michuano hiyo.
Meneja rasilimali
watu,utawala na sheria wa Jambo group
Wakili John Palamagamba Kabudi amebainisha kuwa jumla ya shilingi
million 2 zimetengwa kwa ajili ya mshindi wa kwanza,wapili na watatu huku lengo
la mashindano hayo ni kusaidia watu wenye uhitaji wakiwemo wajane na watoto
yatima.
Wakili John amesisitiza
kuwa upatikanaji wa timu zitakazoshiriki ni kupitia usajili unaoendelea
kufanyika katika ofisi za Jambo FM (Ibadakuli) kwa timu mbalimbali za mitaani
na taasisi kwa gharama ya shilling laki mbili na nusu (Tsh 250,000) na kujipatia seti ya jezi bure.
Sambamba na hayo,
waakili John amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi kwani kiingilio ni
shilingi 500 ambapo kila shabiki atapatiwa kinywaji cha bure kwa kila mchezo.
Michuano hiyo itaanza
kutimua vumbi kuanzia tarehe 14/3/2024 kuanzia saa 3:15 usiku hadi tarehe
3/4/2024.