Na Elisha Petro
Bodi ya Ligi kuu Tanzania imesitisha matumizi ya
uwanja wa Jamhuri uliopo Morogoro kwa matumizi ya michezo ya Ligi kuu NBC
kutokana na mapungufu ya miundombinu inayosaidia urushaji wa matangazo.
Kabla ya uwanja huo kusitishiwa matumizi ulikuwa
ukitumiwa na klabu ya Simba katika michezo yake ya nyumbani ambapo majadiliano
yalifanyika na kufikiwa kwa uamuzi wa kusitisha matumizi ya uwanja huo.
Kwa mujibu wa taarifa ya bodi ya ligi rasmi klabu ya
Simba itatumia uwanja wa Azam Complex uliopo jijini Dar es Salaam na mechi
inayofuata Simba atakuwa nyumbani kuwakaribisha Singida Fountain Gate.
Aidha uwanja wa Jamhuri unaendelea kutumika katika
michuano mingine iliyochini ya TFF ikiwemo Championship na Firstleague