Na Mapuli Kitina Misalaba
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kwa
kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stad VETA wametoa mafunzo ya sheria na kanuni
za usalama Barabarani kwa wajumbe wa kamati ya siasa, kamati za utekelezaji
UWT, Wazazi, UVCCM ngazi ya Wilaya na viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya
kata.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya
ya Shinyanga mjini ambapo mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga
mjini Mhe. Anord Makombe.
Akizungumza na washiriki hao, Mkuu wa Polisi kitengo
cha usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Dezdery Kaigwa ametumia nafasi hiyo
kuwataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, ambao
wameshiriki mafunzo hayo kuwa kielelezo na mfano wa kuzingatia sheria na kanuni
za utumiaji wa vyombo vya moto Barabarani.
Amewataka viongozi hao kuwa mfano wa kufuata sheria
na kanuni za usalama Barabarani kwa watumiaji wengine ili kuepuka ajali
Barabarani.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo kutoka chuo cha
Ufundi Stad VETA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mwambopa Yona pamoja na mambo mengine
ameeleza faida mbambali za mafunzo hayo kutolewa kwa viongozi.
“Unapopata
Elimu ya utumiaji wa chombo cha moto inakusaidia wewe kuendesha chombo chako
ukiwa salama lakini pia ni usalama kwa watu wengine mafunzo haya yanaumuhimu
sana kwa sababu unapopata Elimu maana nake unakuwa na tahadhari ya namna gani
unaweza kuendesha chombo chako cha moto kwahiyo inakusaidia kujilinda”.amesema
Yona
Pia amekiomba Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga na Wilaya zake kuwasaidia kupata wanachuo wengi wanaotoka Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema wanachuo wengi wanaojifunza katika chuo hicho wanatoka nje ya Mkoa wa Shinyanga.
Akifunga mafunzo hayo mgeni rasmi Mwenyekiti wa
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Anord Makombe amewataka
washiriki hao kuzingatia mafunzo hayo ili watu wengine wajifunze kutoka kwao.
Naye kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya
ya Shinyanga Bi. Doris Yotham Kibabi amewataka viongozi hao kuepukana na tabia
ya kuendesha chombo cha moto wakiwa wamelewa.
Kaimu katibu huyo Bi. Doris Kibabi amesema katika
kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni vema kila mmoja kuwa
makini, kuchukua tahadhari ili kuepukana na ajali Barabarani.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo
wamelipongeza jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani na Chuo cha Ufundi
VETA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatawawezesha kuzingatia
sheria na kanuni za usalama Barabarani.
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kwa
kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stad VETA wametoa mafunzo hayo ikiwa ni
mwendelezo wa kufikia makundi mengine.
Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama Barabarani Wilaya
ya Shinyanga Dezdery Kaigwa akitoa elimu huku akisisitiza kuzingatia sheria na
kanuni za usalama Barabarani.

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mafunzo hayo leo
Alhamis Machi 21,2024.

Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Machi 21,2024.
Mafunzo ya sheria na kanuni za usalama Barabarani kwa wajumbe wa kamati ya siasa, kamati za utekelezaji UWT, Wazazi, UVCCM ngazi ya Wilaya na viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya kata yakiendelea katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Machi 21,2024.
Mafunzo ya sheria na kanuni za usalama Barabarani
kwa wajumbe wa kamati ya siasa, kamati za utekelezaji UWT, Wazazi, UVCCM ngazi
ya Wilaya na viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya kata yakiendelea katika
ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Machi 21,2024.

Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya
Shinyanga Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis
Machi 21,2024.