VIONGOZI WA CCM SHINYANGA WAPATA MAFUNZO JUU YA UMUHIMU WA KUZINGATIA USALAMA BARABARANI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stad VETA wametoa mafunzo ya sheria na kanuni za usalama Barabarani kwa wajumbe wa kamati ya siasa, kamati za utekelezaji UWT, Wazazi, UVCCM ngazi ya Wilaya na viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya kata.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini ambapo mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Mhe. Anord Makombe.

Akizungumza na washiriki hao, Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Dezdery Kaigwa ametumia nafasi hiyo kuwataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, ambao wameshiriki mafunzo hayo kuwa kielelezo na mfano wa kuzingatia sheria na kanuni za utumiaji wa vyombo vya moto Barabarani.

Amewataka viongozi hao kuwa mfano wa kufuata sheria na kanuni za usalama Barabarani kwa watumiaji wengine ili kuepuka ajali Barabarani.

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo kutoka chuo cha Ufundi Stad VETA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mwambopa Yona pamoja na mambo mengine ameeleza faida mbambali za mafunzo hayo kutolewa kwa viongozi.

“Unapopata Elimu ya utumiaji wa chombo cha moto inakusaidia wewe kuendesha chombo chako ukiwa salama lakini pia ni usalama kwa watu wengine mafunzo haya yanaumuhimu sana kwa sababu unapopata Elimu maana nake unakuwa na tahadhari ya namna gani unaweza kuendesha chombo chako cha moto kwahiyo inakusaidia kujilinda”.amesema Yona

Pia amekiomba Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga na Wilaya zake kuwasaidia kupata wanachuo wengi wanaotoka Mkoa wa Shinyanga ambapo amesema wanachuo wengi wanaojifunza katika chuo hicho wanatoka nje ya Mkoa wa Shinyanga.

Akifunga mafunzo hayo mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Anord Makombe amewataka washiriki hao kuzingatia mafunzo hayo ili watu wengine wajifunze kutoka kwao.

Naye kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bi. Doris Yotham Kibabi amewataka viongozi hao kuepukana na tabia ya kuendesha chombo cha moto wakiwa wamelewa.

Kaimu katibu huyo Bi. Doris Kibabi amesema katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni vema kila mmoja kuwa makini, kuchukua tahadhari ili kuepukana na ajali Barabarani.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamelipongeza jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani na Chuo cha Ufundi VETA Mkoa wa Shinyanga kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatawawezesha kuzingatia sheria na kanuni za usalama Barabarani.

Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Stad VETA wametoa mafunzo hayo ikiwa ni mwendelezo wa kufikia makundi mengine.

 

Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Dezdery Kaigwa akitoa elimu huku akisisitiza kuzingatia sheria na kanuni za usalama Barabarani.

Mkuu wa Polisi kitengo cha usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga Dezdery Kaigwa akitoa elimu huku akisisitiza kuzingatia sheria na kanuni za usalama Barabarani.

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Machi 21,2024.

Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Machi 21,2024.

Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza kwenye mafunzo hayo leo Alhamis Machi 21,2024.

Mafunzo ya sheria na kanuni za usalama Barabarani kwa wajumbe wa kamati ya siasa, kamati za utekelezaji UWT, Wazazi, UVCCM ngazi ya Wilaya na viongozi wa Chama na Jumuiya ngazi ya kata yakiendelea katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini leo Machi 21,2024.





Previous Post Next Post