WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA BARIADI MKOANI SIMIYU WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA DROIN ZA UMWAGILIAJI KATIKA MASHAMBA YA PAMBA.


Na Swalehe Magesa,Misalaba Media - Bariadi,Simiyu

 

- Wakulima wa zao la Pamba  Bariadi waishukuru  Serikali kwa kuwapelekea ndege isiyokuwa na rubani ( Droin ) kwa ajili ya kupulizia viwatilifu kwenye  mashamba ya pamba.

WAKULIMA wa zao la pamba wilayani Bariadi mkoani Simiyu wameiomba Serikali pamoja na Bodi ya Pamba  kupeleka huduma zaidi ya unyunyuziaji viwatilifu  kwa kutumia Ndege isiyokuwa na Rubani ( DROIN ) katika mashamba kutokana na Teknorojia hiyo kuua wadudu kwa haraka.  


 

Afisa kilimo kupitia Mradi wa BBT chini ya Kampuni ya ( SK ) Masakala Hamis,amesema kupitia Mradi wa kutumia Droin umesaidia wakulima kuthibiti wadudu kwa haraka na muda kidogo kunyunyuzia shamba la hekali nyingi pia umesaidia wakulima kufanya kazi kwa urahisi na kutumia nguvu kazi kidogo.

Afisa kilimo Kata ya Gamboshi kupitia Mradi wa BBT Alexsaimon Kibanyengela amesema, Teknolojia hiyo imewasaidia sana wakulima kufanya kazi kwa ufasaha na kufurahia kilimo tofauti na upuliaziaji wa awali wa kutumia mashine ya kubemba mgongoni ambayo ilikuwa ikiwaletea maumivu makali.


 

Afisa kilimo wa Pamba Saidi Tasso amesema, Teknolojia ya kunyunyuzia mashamba ya pamba kwa kutumia ndege isiyokuwa na rubani imekuja kuwakomboa wakulima wa zao la pamba wenye  mashamba makubwa waliokuwa wakitumia nguvu nyingi kubeba pump mgongoni wakati wa kunyunyuzia viwatilifu.

 

" Lakini kwasasa tuna Teknolojia mpya ambayo inarahisisha kazi na ina uwezo wa kupulizia hekali kumi na tano kwa saa moja tu, kwa kawaida mtu aliyekuwa akitumia Pump ya mgongoni  alipuzia hekali moja kwa masaa matatu hadi manne kwa hiyo hii imekuwa ni mkombozi," Saidi Tasso - Afisa kilimo wa Pamba.


 


 

Previous Post Next Post