Na Swalehe Magesa, Misalaba Media - Itilima Simiyu
Bodi ya Pamba imetoa elimu kwa wakulima wa kijiji cha Kabale wilayani Itilima mkoani Simiyu ya kutengeneza mbolea ya asili inayotengezwa kwa gharama nafuu na itawezesha kilimo cha pamba kuwa na tija zaidi kutokana na mbolea hiyo kusitawisha mazao mengi shambani.
Wakizungumza na Jambo Digital wakulima hao wameipongeza Bodi ya Pamba kwa kuwaletea elimu hiyo, ata hivyo wamesema elimu hiyo wataenda kuifundisha kwa wakulima wengine wa zao hilo ili iweze kuwasaidia wengi zaidi.
" Na kwa namna ambavyo tumefundishwa katika programu hii na wawezeshaji ni jambo la kuwashukuru naamini nikitengeneza kwa gharama ya shilingi laki mbili naweza kupata lita elfu moja itakayo niwezesha zaidi katika kilimo cha pamba kiwe na tija kwangu na kwa wengine," Samwel Benjamin - Mkulima wa kijiji cha Kabale.
Emmanuel Mahandira ambaye ni mkulima wa zao la pamba katika kijiji hicho amesema,wamefurahia mafunzo hayo ya kutengeneza mbolea ya asili kwakua ni teknoljia ambayo wanao uwezo wa kuitengeneza kutokana gharama yake kuwa ndogo zaidi.
" Kwa hiyo tunaishukuru sana Serikali pamoja na Bodi ya Pamba kwa kukumbuka kwamba hizi teknolojia zinapoletwa wanapofundishwa wao na wanakuja kutufundisha leo wameleta haya mafunzo katika kikundi hiki cha Muungano na imani kwamba mbolea hii itafanya kazi vizuri,"Emmanuel Mahandira - Mkulima wa zao la Pamba kijiji cha Kabale.
Afisa kilimo Bodi ya Pamba wilaya ya Itilima Saidi Tasso amesema, teknojia hiyo mpya wameipata kutoka nchi ya BRAZIL ambayo sasa wanatoa mafunzo yake kwa wakulima ili waweze kuitumia katika kilimo cha pamba kutokana kuonekana kuwa na mafanikio zaidi katika kuwaangamiza wadudu shambani.
" Teknolojia hii ni rafiki imekuja kumkomboa mkulima hasa ukilinganisha na mabadiliko ya tabia ya nchi tunaona kumekuwa na mvua nyingi ,mtu anaweza kuwa ameweka mbolea shambani mvua kubwa ikanyesha matokeo yake ile mbolea inazama ndani ya udongo, hii inagusa kwenye mmea moja kwa moja,"Saidi Tassa - Afisa kilimo Bodi ya Pamba wilaya ya Itilima.