WANAWAKE LAKI MOJA SHINYANGA WAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA AGAPE, MKURUGENZI AWAOMBA WADAU KUJITOKEZA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Asasi ya Wanawake laki moja Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imetoa msaada wa chakula katika kituo cha wahanga wa ukatili kinachomilikiwa na shirika la Agape AIDS Control Programme kilichopo kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake laki moja Mkoa wa Shinyanga Annaskolastika Ndagiwe ( MC Mama Sabuni) amesema Asasi hiyo imeguswa baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape kuwa kituo hicho hakina chakula.

Mwenyekiti huyo amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kuwasaidia wahanga hao ili wapate chakula huku akitaja msaada wa vitu alivyokabidhi ikiwemo Unga, Mchele, Maharage pamoja na Sukari.

“Nilipata taarifa asubuhi kutoka kwa Mkurugenzi wa Agape akiniambia kwamba watoto hawana chakula kabisa kwa kweli iliniumiza nakumbuka nilimtumia ujumbe nikamwambai awaambie watoto waingie kwenye maombi wakati mimi ninaenda kuwatembelea ndugu na jamaa namshukuru Mungu wadau niliowatembelea lakini pia wadau waliosoma ujumbe ambao niliusambaza kwenye magroup ya WhatsApp wameweze kuniunga mkono angalau tumepeta chochote”.

“Nimefanikiwa kupata msaada na sadaka kutoka kwa wadau mpaka kufikia sasa nakabidhi vitu vifuatavyo nimepata Unga kilo 80, Mchele kilo 100, Sukari kilo 53, Mahindi ya makande kilo 37, nimepata Maharage kilo 31, nimepata Mboga mboga za kutosha kutoka kwa wadau wangu wa soko la Nguzonane wamenipa Mboga mboga zenye thamani ya elfu ishilini (20000)”.

“Nimepata Nyanya ntole, Kabechi, Bamia, Bilinganya, Pilipili, Limao Nyanya, Vitunguu, Chumvi pakiti tatu, Dagaa sado moja, pamoja na Mafuta lita tatu vyote hivi jumla ya thamani yake ni shilingi laki sita naomba niwashukuru wadau wote ambao leo wametoa Mungu awabariki sana”.amesema Mwenyekiti Annaskolastika

“Niwaomba wadau wote wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kujitolea ili kupunguza changamoto iliyopo chochote ulichonacho we niite au nitumie kwenye simu kitawafikia niwakumbushe wananchi wa Manispaa ya Shinyanga hiki kituo ni cha kwetu naomba tunyenyuke kwa Miguu yetu miwili tutembelee kituo hiki na tuweze kuwasaidia hakuna kitu kilichoniumiza leo kukuta na mtoto mwenye umri wa Miaka kumi na tatu mjamzito hajui mimba amebeba lini  hajui mtoto wake anamiezi mingapi imenisikitisha, imeniumiza anadamu saba na yupo hapa kituoni ambapo Myula analia kwamba hakuna chakula ebu fikiria anapata wapi chakula cha kuongeza damu”.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika la Agape AIDS Control Programme ambaye pia ni msimamizi wa kituo kinacholea watoto waliopitia ukatili wa kijinsia Bwana John Myola amewashukuru Wanawake laki moja na wadau mbalimbali walioguswa ambapo amesema pamoja na changamoto zingine uhitaji wa chakula ni mkubwa huku akiwaomba wadau kuendelea kujitokeza kusaidia kituo hicho.

“Ninaomba nitoe shukurani zangu za dhati na za muhimu kwa Wanawake laki moja ambao wametuletea chakula kwa kweli niseme wote waliohusika Mungu akawabariki  sana kwa kile mlichokitoa maana hii leo kweli tulikuwa hatuna hata chakula, naomba niwaombe wadau wengine wasamalia wema watanzania wenzetu wawaone hawa watoto kituo kina takribani watoto 40 na kikubwa zaidi hawa watoto ni watoto ambao wametendewa ukatili kwa sasa sisi wengine ebu tusimame tuwasaidie watoto hawa”.

“Mimi sina mfadhili wa aina yoyote tangu Mwaka 2016 kuna muda nilitumia vifaa vya familia nilitumia mali za familia kwahiyo inafika hatua na mimi naanza kuchoka imekuwa ni ngumu lakini nasema hili nalo litapita lakini niwaombe sana sana watanzania wenye mapenzi mema watusaidie sisi hata shilingi Mia tano nikubwa sana tutanunua pakiti ya Chumvi siku itapita kuliko kukosa kabisa kwahiyo naomba niseme kwa yoyote mwenye chochote asiseme ni kidogo kwetu chochote kinachotumika kwenye mwili wa binadamu hasa chakula lakini pili tunahitaji walimu maana kuna watoto ambao wanahitaji kusoma masomo ya sekondari kwahiyo tunaupungufu au tunashida kubwa ya walimu”. Amesema Bwana Myola

Unaweza kuwasiliana moja kwa koja na Mkurugenzi wa shirika la Agape 062 3528183

Au wasiliana na MC Mama Sabuni kwa namba ya simu 0767500455


 

Previous Post Next Post