WANAWAKE MKOA WA SHINYANGA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga wameiomba Serikali kuendelea kutatua kero na kushughulikia changamoto zinazowakabili katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji Wanawake kiuchumi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni katibu wa jukwa hilo Taifa  Dkt. Regina Malima wakati akisoma risala kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Shinyanga imefanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga.

Mwenyekiti huyo pamoja na mambo mengine ameiomba serikali kuendelea kuchukua hatua kali kwa watu wote wanaobainika kuhusika katika vitendo vya kikatili dhidi ya Wanawake na watoto huku akiomba kuharakisha zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa wanawake, vijana na makundi maalum.

“Sisi Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga tunaiomba Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hasssan kuendelea kuchukua hatua kwa kutatua changamoto zinazowakabili Wanawake kuendelea kutoa Elimu ya uwezeshaji kiuchumi sambamba na kuharakisha utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa Wanawake, Vijana na Makundi maalum, Lakini pia Elimu ya siasa na uongozi iendelee kutolewa kwenye mikusanyiko mbalimbali hasa maeneo ya vijijini ili tuweze kupata uwakilishi mzuri katika ngazi mbalimbali za uongozi hususan kwenye agenda zinazohusu Wanawake”.

“Tunaiomba Serikali kuendelea kuchukua hatua kali na stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi kwa wote wanaohusika katika vitendo vya kikatili dhidi ya Wanawake na Watoto pia Serikali ihakikishe kuwa mila zinazokandamiza Wanawake zinaondoka na hivyo kujenga jamii yenye maadili yenye usawa lakini pia Serikali ichukue hatua kwa wale wote wanaojihusisha na kuwakopesha Wanawake mikopo yenye riba kubwa (kausha Damu) kinyume cha sheria na taratibu za Nchi ili kunusuru Wanawake wengi walioathirika na mikopo hiyo”.amesema Dkt. Regina

“Kwa niaba ya Wanawake wote wa Mkoa wa Shinyanga tunaahidi kushirikiana na Serikali kwa kuja na mikakati mbalimbali ya kuwakomboa Wanawake katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, kielimu, kiafya na kiutamaduni ili waweze kusonga mbele katika ustawi wa maendeleo na pia tunaahidi kuchapa kazi kwa viwango ili kuendelea kutetea heshima kubwa ya Mkoa wetu na Taifa “.

“Sisi Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kwenye masuala yanayohusu Wanawake hasa katika sekta ya Afya na sekta zingine kwani kupitia uongozi wake ametuheshimisha na kuidhihirisha Dunia kuwa Wanawake tunaweza kushika nafasi yoyote na kuleta mabadiliko makubwa’.amesema Dkt. Regina

Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesisitiza wanawake kushirikiana katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika juu ya vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika jamii.

Misalaba Media imezumgumza na baadhi ya wanawawake walio hudhuria maadhimisho hayo ambapo wamesema licha ya mafanikio waliyoyafikia lakini bado kuna changamoto zinazowakabi hasa katika suala la uchumi ambapo wameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa mikopo yenye riba nafuu inayotolewa na Halmashauri.

Aidha katika maadhimisho hayo, Wanawake wafanyakazi Mkoa wa Shinyanga (TALGWU)  wamekabidhi msaada wa chakula kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika shirika la Agape AIDS Control Programme huku Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Shinyanga (TPF- NET Mkoa wa Shinyanga) wakikabidhi mifuko 31 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Bweni katika shule ya watoto wenye mahitaji Buhangija Manispaa ya Shinyanga.

Maadhimisho ya siku ya wanawake hufanyika kila ifikapo Machi 8 kila Mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema “WEKEZA KWA WANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII”

Siku ya Wanawake Duniani ina historia yake na ilianza kuadhimishwa Machi 8 Mwaka 1975 baada ya umoja wa mataifa kuridhia siku hii kuwa siku rasmi ya kuikumbusha Dunia juu ya haki za Wanawake, kusherehekea siku hii kumekuwa kukiongeza chachu katika harakati za mapambano katika kufikia usawa wa kijinsia kwa Wanawake na Wanaume katika jamii.

Kwa kutambua umuhimu wa sikuu kuu hii, Nchi yetu pia imekuwa ikitambua umuhimu wake na hivyo kushirikiana na Wanawake na jamii kwa ujumla katika kusherehekea ikiungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku hii.

   

Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji Wanawake kiuchumi Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni katibu wa jukwa hilo Taifa  Dkt. Regina Malima akisoma risala kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanya kwenye uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024.

               

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanya kwenye uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanya kwenye uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita  akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanya kwenye uwanja wa Sabasaba Kambarage mjini Shinyanga leo Ijumaa Machi 8,2024.






Zoezi la Wanawake wafanyakazi Mkoa wa Shinyanga (TALGWU)  kukabidhi msaada wa chakula kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika shirika la Agape AIDS Control Programme likiendelea.

Kituo hicho bado kinakabiliwa na changamoto ya chakula ambapo Mkurugenzi wa shirika la Agape AIDS Control Programme ambaye pia ni msimamizi wa kituo kinacholea watoto waliopitia ukatili wa kijinsia Bwana John Myola anaendelea kuwaomba wadau kujitokeza ili kupunguza changamoto iliyopo.

Unaweza kuwasiliana moja kwa koja na Mkurugenzi wa shirika la Agape 0623528183

Au wasiliana na MC Mama Sabuni kwa namba ya simu 0767500455


Previous Post Next Post